Mtaa Kwa Mtaa Blog

June 2011
1 AFRICANLYON AFYA AIRTANZANIA AJALI AJIRA ARUSHA ATCL AZAMFC BARABARA BEACH SOCCER BIASHARA BIASHARA. BU BUNGE BUNGENI BURUDANI BURUNDI CCM CHADEMA CONGOBR DAR ES SALAAM DARAJA LA KIGAMBONI DAWA ZA KULEVYA DAWASCO DINI DODOMA EAC EID ELIMU EPL FEDHA NA UCHUMI FILAMU GAMBO GOFU H HABARI HABARI KIJAMII HABARI MCHANGANYIKO HABARI MICHEZO HABARI ZA BIASHARA HABARI ZA NYUMBANI HALI YA HEWA HARUSI HIFADHI HIFADHI. HISTORIA IBADA IKULU JAMII JESHI JESHI LA POLISI JK JKT-RUVU KAGERA KAGERA SUGER KAITABA KAMERA YA MTAA KWA MTAA KANDA YA ZIWA KARATE KARIAKOO KAZI KIFO KIGOMA kijamii KILIMANJARO KILIMO KIMATAIFA KITILYA KUMBUKUMBU KUOGELEA KUPATWA KA JUA KUPATWA KWA JUA KUTOKA BUNGENI LOWASSA LYON MAAJABU MADAWATI MADINI MAENDELEO MAFUNZO MAFUTA NA GESI MAGAZETI MAGEREZA MAHAFALI MAHAKAMA MAISHA MAJI MAJIMAJI MAKAL MAKALA MAKALA MICHEZO MAKAMU WA RAIS MAKONDA MALIASILI MAPATO MAREKANI MASUMBWI MATANGAZO MATUKIO MATUKIO MTAANI MAWASILIANO MAZINGIRA MBAOFC MBEYACITY MESSI MGAMBO MICHEZO MICHEZO. MIFUGO MIFUKO YA JAMII MISS TZ MITINDO MIUNDOMBINU MOROGORO MSIBA MTAA KWA MTAA TV MTIBWA MUHAS MUZIKI MWADUI MWANZA NANENANE NDONDO NHC NIDA NISHATI NYEREREDAY PICH PICHA PPF PRISONS RAIS MAGUFULI RATIBA RIADHA RUVU SADC SANAA BURUDANI SANAA NA UTAMADUNI SERENGETIBOYS SHEREHE SHERIA SIASA SIKUKUU SIMANZI SIMBASC SIMULIZI SOKA SONGWE TAHADHALI TANGA TANZIA TBL TEKNOLOGY TEKNOLOJIA TETEMEKO TRL TTCL TUZO UBUNIFU UCHAMBUZI UCHUKUZI UCHUMI UFARANSA UFUGAJI UGANDA UHURU DAY UJASILIAMALI UJENZI UK UKUTA ULAYA UMOJA WA TAIFA UREMBO USAFIRI USALAMA UTAFITI UTALII UTAMADUNI UTURUKI UWEKEZAJI VIJANA VIOJA VIUMBE VIWANDA VODACOM VPL WANAWAKE WAREMBO WASANII WATOTO WATU WAWAKILISHI WAZEE WAZIRI MKUU YANGA ZANACO ZANZIBAR ZIMAMOTO

The recent announcement by government through Prime Minister Mizengo Pinda of expenditure estimates for 21 regions and 133 districts for the fiscal year 2011/12 provides a dim light at the end of a dark tunnel when it comes to fighting unnecessary expenditures. The presentation shows some reduction in unnecessary spending such as travel expenses, acquisition of new vehicles and so on.

Sikika's analysis of the presentation shows that all unnecessary budget items sum up to about Tsh 30.4 bn, which is about Tsh 7.8 bn, or 20 percent, less in comparison with the last financial year’s budget where those items summed up to Tsh 38.3 bn. This commendable development can mainly be attributed to the cuttings of travel expenses which have been reduced from Tsh 10.9 bn in the 2010/11 to Tsh 8.3 bn year 2011/12, that’s a decrease of 24 percent. 

Trainings have also been successfully reduced from Tsh 2.3 bn to Tsh 1.9 bn, implying a decrease of 19 percent. Both expenditures on hospitality supplies and on fuel, oils and lubricants are also cut down by about 20 percent. The allocations for new vehicles drop from Tsh 2.9 bn to Tsh 1.1 bn; this is Tsh 1.8 bn or 63 percent less than the previous year.

Overally, these budgetary reductions across regions are truly remarkable. They show that the government is starting to implement what the Prime Minister proclaimed in 2008 when he announced a refocus to activities that benefit the general populace, particularly in rural areas where the bulk of the Tanzanian population lives, rather than concentrating on ineffective activities like seminars, workshops and the acquisition of expensive vehicles. Moreover, the Minister of Finance reemphasized, on the 8th of June 2011, that “the government will continue with its efforts to control expenditure by suspending procurement of all kinds of vehicles except for special reasons; and with approval of the PM’s office”.

Sikika takes this opportunity to congratulate the Prime Minister for adhering to his own and the Minister of Finance’s statements by reducing unnecessary expenditures – in particular regarding the acquisition of new vehicles. But, at the same time, raises the following concerns: 14 out of 21 regions did not budget for vehicles at all calling the sustainability of this financial development into question.

 If these regions just postponed the purchasing of vehicles for one year, as the Minister announced, they will budget for those expenditures in the coming financial year. But what matters is not a total elimination of such costs; rather it is to ensure that public funds are spent economically and bring value for money. Thus, we would prefer to have the government purchasing favourable vehicles which ‘do the job’ instead of pricy Land Cruisers and SUVs.

In total, the regions managed to save almost eight billion Tsh by cutting down unnecessary activities. This raises the question where this huge amount is diverted to. Sikika insists on redirecting more money to the health sector whose budget stagnates while all other key sectors are receiving more than in the previous year.

Sikika is also of the view that though considerable progress has been made in as far as fighting unnecessary expenditures is concerned, the government should do more as the figures are still unreasonably high. The government should also desist from lip service and diligently implement all measures meant to reduce unnecessary spending for the benefit of the general public.

 Nape Nnauye akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers katika chumba cha habari cha Global. Wengine ni Mrisho, Ndauka, sixtus na Ally.
 Nape akiwa katika ofisi za Global Publishers. Kushoto ni  Abdallah Mrisho Wengine kutoka kulia ni, Sixtus Mapunda, Maloto,Ndauka na Mhariri kiongozi wa michezo wa Global Saleh Ally
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Kiu, Ijumaa na Champion, Abdallah Mrisho, baada ya kuwasili Ofisi za kampuni hiyo,Mwenge, Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mhariri Kiongozi wa kampuni hiyo  Oscar  Ndauka na Mwandishi wa kampuni hiyo Luqman Maloto na wapili kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.
 Mhariri wa Citizen wa Bakari Machumu akimpatia maelezo Nape, kuhusu bodi ya uhariri ya gazeti hilo ambavyo hujindaa. Kulia kwa Nape ni Makunga na wengine ni wajumbe wa bod ya uhariri wa gazeti hilo wakiwa kikaoni.

Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipofaya ziara katika ofisi za kampuni hiyo, Tabata Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda na  Kshoto ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga, Mhariri Mrendaji gazeti la Mwananchi Dennis Msacky, na Mhariri wa Mwanaspoti Frank Sanga. 
Nape akionyeshwa maandalizi ya gazeti la Mwananchi katika hatua ya mwisho kabla ya kwenda kuchapwa mtamboni. Anayempa maelezo ni Mhariri Mkuu wa Mwananchi Bw. Theophil Makunga.

Kikosi cha Yanga

 
 Kikosi cha Elman 
 Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Davies Mwape akiwa katika harakati ya kumtoka beki wa Elman,Badri Mo'Alim katika mchezo wa Mashindano ya Kagame-Castle Cup uliochezwa jioni hii ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Wachezaji wa Timu ya Elman ya Somalia,Mohamed Abukar (kushoto) na Said Mohamed (kulia) wakiwania mpira na Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Yanga,Kigi Makasi (kati) katika mchezo wa Mashindano ya Kagame-Castle Cup ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Mwape wa Yanga akiwa chini mara baada ya kufunga bao zuri sana kwa kichwa kutokana na Kipa wa timu Elman kuuteme mpira uliopigwa na Julius Mrope.
Hatari langoni mwa Elman ya Somalia.
Sehemu ya Mashabi wa Yanga waliofurika ndani ya uwanja wa Taifa leo kuisapoti timu yao.

Meneja wa kinywaji cha Grand Malt bidhaa ya TBL ambao ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ya filamu Tanzania (Tanzania Open Film Festival),Consolata Adam akizungumwa wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania linaloendelea katika Viwanja vya Tangamano mkoani Tanga.Wengine pichani ni Meya wa Jiji la Tanga,Mstahiki Mzamil Shemdoe (katikati) na kulia  ni Mkurugenzi wa Sofia Production na Mratibu wa Tamasha hilo,Mussa Kissoky.
Meya wa jiji la Tanga,Mstahiki Mzamil Shemdoe (katikati) akizungumza machache wakati wa ufinguzi wa Tamasha la Wazi la Filamu katika Viwanja vya Tangamano,Mkoani Tanga.
Wana wa Ngoma Baikoko wakionyesha umahiri wao wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wazi la Filamu mkoani humo.
Tamasha la wazi la filamu Tanzania: Grand Malt Open Film Festival limezinduliwa rasmi katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga,kama inayoonekana katika picha.. Wiki ya maonyesho ya wazi ya Filamu inaendelea mpaka tarehe 3 July. Maonyesho hayo ya Filamu yanafanyika kwa mara ya tatu katika historia yake.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mavis Lengalenga, baada ya mazungumzo wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, John Mutinda Mutiso, wakati alipofika kumtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan Nchini Tanzania, Abdelbagi Hamdan Kabeir, wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo  na kufanya mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani - OMR 

Na. Boniphace Makene.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumanne Juni 28, 2011 ametembelewa na Mabalozi wa nchi tajwa hapo juu ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Ziara ya kwanza ilikuwa ya Balozi wa Sudan  Abdelbagi Hamdan Kabeir ambaye alifika kwa lengo la kumsalimia Makamu wa Rais huku pia akitumia fursa hiyo kumuaga kufuatia muda wake wa kushika wadhifa huo hapa nchini kufikia mwisho.


 Balozi Kabeir alifafanua kuwa maisha yake nchini Tanzania yamemfanya kuifahamu nchi yetu na anashukuru kwa ushirikiano wa wananchi wa Tanzania hali inayompa fursa sasa kuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini kwao.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimshukuru Balozi Kabeir kwa kazi nzuri na hasa katika sekta ya elimu ambapo Watanzania kadhaa wamepata nafasi za kusoma nchini Sudan, huku pia nchi hiyo ikisaidia katika sekta ya elimu na kubadilishana wataalam wa sekta hiyo nchini. 

Pia Makamu wa Rais alifafanua kuwa, binafsi angependa kuona kura ya maoni iliyopigwa na kufanikisha kuundwa kwa nchi mpya Sudan Kusini inaheshimika na hivyo Sudan kuwa eneo la amani tofauti na ilivyokuwa huko nyuma. 

Balozi Kabeir alimshukuru Makamu wa Rais na kisha kumuelezea kuwa wao kama Sudan wana mengi ya kujifunza katika kudumisha amani na akatumia mfano wa Zanzibar kama eneo ambalo Tanzania imeonyesha uwezo wake wa kumaliza kero za ndani kwa kutumia watu wa ndani kujadiliana na kukubaliana.

Kwa upande wa Balozi wa Kenya nchini; John Mutinda Mutiso yeye naye alitoa salamu za watu wa Kenya nchini kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye tangu achaguliwe katika wadhifa huo.

 Balozi Mutiso alimueleza Makamu wa Rais kuwa; Kenya inajifunza mengi kutoka Tanzania na akasifia namna Tanzania ilivyoendesha uchaguzi mkuu uliopita, huku akisema wao Kenya kila inapokaribia uchaguzi vidonda vyao vinaibuka na wananchi wanakuwa na hofu ya usalama wao wakati wa uchaguzi. 

Pia Balozi Mutiso alisifia kitendo cha Tanzania kutumia vyombo vya dola katika kuchunguza rushwa katika uchaguzi kwa kuanzia na kura za maoni katika vyama akasema jambo hili halifanyiki Kenya na wao wameona ni jema ambalo wangependa kuliiga.

Balozi Mutiso alimuomba Makamu wa Rais kukuza mashirikiano hasa katika eneo la Mazingira huku na akiielezea Tanzania kuwa iko juu katika utunzaji wa mazingira kulinganisha na Kenya na akamuomba Makamu wa Rais kama ataweza kuwa muda katika ratiba zake kuitembelea Kenya na kuhamasisha upandaji miti.

“Eneo kubwa ambalo Tanzania inaweza kutusaidia ni katika kupata miche ya miti. Tunahitaji kupanda miti kama milioni 100 na uwezo wetu wa kupata mbegu na miche ni mdogo kwa kuwa miti yetu mingi tumeitumia na sasa tunaumia,” alisema Balozi Mutiso.

Balozi huyo pia aliwataka Watanzania kuwa na subira na kuondoa jazba katika suala la kuandika Katiba mpya kwa kuwa wao Kenya iliwachukua miaka 20 hadi kupata katiba waliyonayo leo. “Zoezi hili ni gumu na linahitaji umakini. Hakuna watu kulitumia kwa sababu zao za kutafuta madaraka. Katiba ya nchi inapaswa kuwawakilisha watu wote na hasa walioko vijijini hivyo haiwezi kuandikwa kwa kukimbizana,” alisema Balozi Mutiso.

Makamu wa Rais alimshukuru Balozi wa Kenya na kumuahidi kufanya naye mazungumzo zaidi ya mashirikiano katika sekta ya mazingira hasa baada ya kikao hiki cha Bunge la Bajeti kumalizika.

Kwa upande wake Balozi wa Zambia nchini; Mavis Lengalenga Muyunda yeye alimshukuru Makamu wa Rais na wananchi wa Tanzania kwa ushirikiano wao katika kipindi hiki cha msiba wa kitaifa nchini Zambia, msiba wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Frederick Chiluba aliyezikwa jana. 

Balozi Muyunda alimuelezea Makamu wa Rais kuwa Zambia inathamini uhusiano wake na Tanzania na kwamba inaheshimu nafasi ya Tanzania katika utunzaji na uhifadhiji amani katika ukanda huu wa nchi za Kusini wa Afrika. 

Tena alifafanua kuwa kwa namna alivyofika Tanzania amebaini kuwa ni nchi yenye mikakati na akafafanua kuwa mfano wa kwanza ni bajeti ya mwaka huu ambayo inalenga kutoa majibu katika vipaumbele vinavyowagusa wananchi.

Kuhusu vyombo vya kiuchumi vinavyounganisha Tanzania na Zambia kama TAZARA, TAZAMA NA MOFET, Balozi Muyunda alisema nchi yake inaendelea na jitihada za kuiboresha TAZARA ambapo huko wameshapata mkopo toka China wenye lengo la kuboresha chombo hicho muhimu kwa usafirishaji wa ukanda wa Kusini.

Kwa upande wa Makamu wa Rais alimtakia kila la heri Balozi Muyunda hasa sasa ambapo Zambia inaingia katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba ama mwanzoni mwa Oktoba. 

Pia alimsisitizia kuhusu umuhimu wa nchi hizi kuheshimu mambo mazuri waliyoyaanzisha waasisi wa nchi zetu mbili na kuhakikisha kuwa wanayafunza kwa vizazi vijavyo vya nchi hizi ili kuzidisha moyo wa kuthaminiana na kupendana kwa nchi zote mbili.

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi- Zanzibar


Serikali imewaonya vikali Maafisa na Askari Polisi wanaoendeleza vitendo vya kudai na kupokea rushwa hapa nchini na kuwataka wajiondoe wenyewe kwenye nafasi zao katika Jeshi hilo la sivyo watatolewa kwa nguvu kwa kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa onyo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibar Mh. Haji Omar Kheri, wakati akifunga Mafunzo ya Uongozi Mdogo kwa Askari Polisi yaliyomalizika leo kwenye Chuo cha Polisi Zanzibar.

Akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi ngazi ya Koplo, Sajenti na Sajin-meja, Mh. Kheri amesema pia kuwa hali ya kutowajibika kwa baadhi ya Askari na watendaji wengi wa serikali ni mambo yanayokwenda kinyume na utawala bora.

Amesema kutotenda ama kuchelewesha haki, kudai na kupokea rushwa na kutowajibika ama kutoa siri za wasiri wa Polisi wanaowataja wahalifu, ni mambo yanayoweza kupunguza imani ya Jeshi hilo mbele ya wananchi.

Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi kwa kushirikiana na Serikali ya Muungano zitahakikisha zinatafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili askari kama vile uchakavu wa vituo vya Polisi, ukosefu wa nyumba za kuishi pamoja na ukosefu wa vyombo vya usafiri na mawasiliano ili kuwawezesha kufanya kazi zao kikamilifu.

Akizungumzia mabadiliko ya hali ya uhalifu duniani, Mh. Kheri amesema kuwa mbinu mpya zimekuwa zikibuniwa na wahalifu katika kutekeleza matukio ya kihalifu na hivyo pasipo mafunzo zaidi kwa askari Polisi, haitawezekana kuwakabili kikamilifu.

Hata hivyo Mh. Kheri amepongeza utaratibu unaotumiwa na Jeshi la Polisi hapa nchini wa kutoa mafunzo kabla ya kuwapandisha vyeo wanaostahili na kusema kuwa utaratibu huo unawawezesha askari kukumbushwa wajibu wao wakiwa katika vyeo na madaraka yao mapya.

Hata hivyo Waziri Kheri amesema kuwa ni muhimu kwa kila askari kusaidia katika kuwaelimisha wananchi kufuata misingi ya utawala bora na pia Polisi waepuke kuibua malalamiko kwa kutowatendea haki walalamikaji wanapofika katika vituo vya Polisi jambo ambalo amesema ni kinyume na matarajio ya utawala bora.

Naye Kamishna wa Piolisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa kuanzishwa kwa mpango wa Utii wa Sheria pasipo Shuruti, kumeingizwa katika miradi ya Polisi Jamii na kupunguza matumizi ya nguvu katika ukamataji wa watuhumiwa.

Wakitoa tathimini ya mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar ACP Maulidi Mabakila na Mkufunzi Mkuu wa Chuo hicho SSP Andrew Mwang’onda wamesema kuwa washiriki wote wamefundishwa mambo mbalimbali yatakayoweza kuongeza tija kwa Jeshi la Polisi mbele ya wananchi.

Mkuu wa chuo hicho ACP Mabakila, amesema kuwa wahitimu hao wakiwa chuoni hapo wamepata mafunzo mbalimbali ya ndani na nje ya darasa kama vile kutembelea katika shehia mbalimbali kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa Polisi jamii na Ulinzi shirikishi kwa vitendo wakiwa katika mabaraza ya kamati za Ulinzi na Usalama za Shehia husika.

Kwa upande wake Mkufunzi Mkuu wa Chuo hicho SSP Anderw Mwang’onda, amesema kuwa katika kufanikisha mafunzo hayo Chuo hicho kimewaalika wataalamu mbalimbali kutoka nje na ndani ya Zanzibar ili kutoa elimu itakayowasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao pindi warudipo vituo mwao.

Awali Waziri Kheri alikagua gwaride na kutunuku vyeti na zawadi ya virungu vya heshma kabla ya kuwavisha vyeo wahitimu waliofanya vizuri zaidi wakati wa mafunzo yao kabla ya gwaride kupita mbele yake kwa mwendo wa pole na wa haraka kwa kutoa heshima na baadaye kuona onyesho la judo na singe.

Jumla ya Askari 826 wakiwemo wa mafunzo ya koplo, sajenti na Sajin-meja wamehitimu mafunzo yao ya awamu ya pili chuo hapo.

Mwenyekiti wa Boy George Promosheni Yusuph George, ambao ni waandaji wa shindano la miss Kinondoni akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi na kutoa muuongozo kwa warembo waliofanikiwa kuingia katika kambi hiyo inayoanza rasmi jumatano wiki hii Mzalendo Pub Makumbusho,kushoto ni Afisa udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.

Afisa udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude akiwasalimia baadhi ya warembo wanaoshiriki miss Kinondoni wakati walipotambulishwa rasmi jana tayari kwa kuanza kambi yao siku ya jumatano wiki hii Mzalendo Pub Makumbusho jijini Dares Salaam.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaonyesha waheshimiwa wabunge Kombe ambalo Ofisi ya Bunge imeshinda katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha taasisi mbalimbali za Umma kutoka barani Africa na kufikia kilele wiki iliyopita tarehe 23 Juni, 2011. katika Maonyesho hayo Ofisi ya Bunge imekuwa mshindi wa Pili katika nafasi ya banda bora kwa utoaji bora wa huduma hususani katika kuelezea Kazi Bunge, Muundo wake, Mamlaka ya Bunge nk. picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Waandamaji Majuu wakipinga uhuni waliofanyiwa Watanzania kutoka kwa BAE
Salam,

Desemba mwaka jana SFO (Serious Fraud Office) Uingereza iliiamuru  kampuni ya BAE Systems inayouza vifaa vya ulinzi ulimwenguni kulipa faini kama adhabu ya shughuli zake mbovu za kibiashara na serikali za Saudi Arabia na Tanzania. Mwezi Februari 2011 BAE ilikubali sharti ambalo ni kuilipa SFO paundi milioni 285 na serikali ya Tanzania paundi 29.5 milioni (shilingi 75.3 bilioni), kama pesa za kujisafisha uso; ikiwa ni kuueleza ulimwengu mzima kuwa kampuni hiyo tajiri yenye wafanyakazi laki moja duniani, ina maadili mema.
Toka tamko litokee imezuka migogoro kadhaa.

Bonde moja wamesimama wananchi Bongo wasioamini viongozi  kwamba wana malengo ya kutetea maslahi yao. Hapo hapo, BAE Systems imetoa kauli kwamba pesa  ziende kwenye mashirika ya fadhila( na NGO) Tanzania ambayo kawaida ni ya kigeni. Imedaiwa barua zimeandikwa na wananchi kuiomba BAE isiipe serikali pesa hizo.

Kilima kingine wamekaa wabunge na viongozi wa serikali wanaoamini huu ni ukoloni mambo leo. Kwamba nchi tajiri kuiamuru nchi changa namna ya kufanya mambo yake ni utumiaji mabavu kiuchumi.

Kihistoria baada ya Waafrika kutawaliwa miaka zaidi ya 60 tuliachwa maskini na wale waliojali maslahi ya raia waliondolewa na Wazungu, mathalan Patrice Lumumba wa Kongo alieuawa 1961 na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Mobutu. Toka Jenerali Mobutu alipochukua madaraka mwaka 1965  hadi leo Kongo-Zaire imeharibiwa kabisa.

Wapo waliomudu kama Mwalimu Nyerere aliyetetea Uafrika na kujenga amani Tanzania ambayo tunayo hadi leo.

Toka habari kuhusu Wabunge wanne kuja Uingereza kuzungumzia mtafaruku huu  chuki na hasira iliyoenea kutokana na ufisadi ni kama imewashwa; kidonda kimetoneshwa. Mhusika mmojawapo wa tukio la 1999,  Shailesh Vithlani ambaye inadaiwa alipewa hongo kutimiza dili, hajulikani aliko. Hata baada ya mahakama ya Uingereza chini ya Justice Bean kuamuru ashtakiwe bado bwana Vithlani yadaiwa anajificha Uswisi.
Balozi Uingereza, Mhe Peter Kallaghe (wa pili) alipowakaribisha Wabunge na ofisa wa mawasiliano kukutana na wanahabari. wanne kulia ni kiongozi wa msafara, Naibu Spika wa Bunge la Taifa, Mhe Job Ndungai.
Je, tutajuaje kwamba Wabunge wetu wanalo zuri moyoni, wanauliza wasomaji wengi mitandaoni? Je wahusika wengine katika dili hilo ambao bado wako serikalini wamefikia wapi? Je, tutaamini vipi kwamba mabilioni haya ya Waingereza yatatumiwa kusaidia elimu ya watoto wetu nchini, kama wanavyoahidi?
Hatuwezi kujua. Tunaloweza kulifanya ni kuamini. Kwa vipi?

Wakiongea katika Ubalozi wetu Uingereza mjini London, juma lililopita viongozi hao chini ya Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai walihimiza  kuwa wanafuatilia matokeo ya mahakama ya sheria Uingereza inayochunguza rushwa (SFO) maana kadri muda unavyokwenda ndivyo riba inaongezeka.

Kampuni ya BAE systems huuzia ulimwengu mzima silaha mbalimbali za ulinzi wa majini, ardhini na anga, pia vifaa vya kisasa  vya mawasiliano ya habari, umeme, usalama na teknolojia. Mwaka jana BAE systems ilipata faida ya paundi bilioni 22.4 (takribani shilingi trilioni 60).

Wabunge walikutana na “House of Lords” ambacho ni kitengo cha juu Bunge la Uingereza chenye usemi mzito nchi hii ya Malkia. Walikutana pia na Wabunge wenzao akiwemo Naibu Spika wa Bunge Lindsay Hoyle. Walitegemewa pia kukutana na maofisa wa kampuni ya BAE Systems Philip Bramwell na Lesley Collen.

Mbunge, John Momose Cheyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayohusika na Hesabu za Umma, aliwahakikishia wanahabari kwamba katika miaka kumi toka tukio hilo la 1999 vyombo vya serikali dhidi ya rushwa vimebadilika na kuimarika. “Matumizi halali ya fedha yatakahakikisha pesa zitatumika kujenga elimu,” alisema mwakilishi huyu wa Bariadi Mashariki.
Wabunge walionyesha nia ya kutaka kusafisha jina la Tanzania, kurekebisha jina la viongozi wetu na kuleta sura mpya ya mambo yanayoiharibu Afrika.

Walisisitiza na kuahidi kinaga ubaga kwamba pesa zitaendeleza elimu. Kauli yao ina maana macho yote yanawatazama na kuwategemea kama mashujaa wapya. Tusiwahukumu kabla hata ya kuanza.

Itakuwa vyema tukiikubali kauli yao kuwa wanadhamiria kutumia nafasi yao walioipatia kupitia kura za kidemokrasia kutenda la maana. Hakuna haja ya kumzomea mtu anayejaribu uzuri. Mwache kwanza amalize anachokidhamiria kabla ya kupiga kelele. La maana kwa sasa ni kuwatakia kheri maana kuna mawili. Nchi yetu kudharauliwa na wageni na  huduma mojawapo muhimu nchini, yaani elimu, kukidhiwa.
  
 Sasa hivi kweli tukibadilishana meza, tuseme Tanzania ndio tuwe na uwezo wa kufanya utapeli kwa kuwauzia rada Waingereza? Kisha  baadaye watushtukie kuwa tulifanya rafu?  Halafu sisi tuwaambie kuwa tutawalipa baadhi ya fedha kutumia NGOs zetu?  Je, tutakuwa salama? Je mnadhani Waingereza wataukubali usanii huo?

MGOGORO WA RADA ZA NDEGE BAINA SERIKALI NA BAE SYSTEM UNAWEZA KUWA CHANZO CHA UONGOZI BORA TANZANIA

Tafakari.

Asanteni,

Imeandikwa na Freddy Macha pamoja na URBAN PULSE 
wakishirikiana na Jestina George

Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Ngoma za Asili Mkoani Kagera,Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba,Mh. Ndyamukama akihutubia washiriki wa Mashindano ya Ngoma za Asili yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Balimi Extra lager, kushoto ni Andrew Mbwambo Meneja Mauzo na Erick Mwayela, Meneja Matukio kanda ya ziwa.
Mshindi wa kwanza Mashindano ya Ngoma za Asili kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba aliepokea fedha taslim laki tano (500,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Ndyamukama akisalimiana na Andrew Mbwambo Meneja Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania. Mshindi wa pili katika mashindano hayo kilikuwa ni kikundi cha Rugu toka Karagwe walijipatia laki Nne(400,000/=), wa tatu ni Kabale toka Manispaa ya Bukoba walijipatia laki tatu(300,000/=).
Kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza.
Kundi la Rumanyika kutoka Karagwe wakionyesha umahiri wao wa ngoma za asili.
Hivi ndivyo mambo yalivyokua katika viwanja vya Kaitaba katika kumsaka mshindi wa mashindano ya ngoma za asili kupitia kinywaji cha Balimi Extra lager.


Makundi mbalimbali yakionyesha umahiri wao.

Vikombe vya Ushindi.
Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Siylvia Lupembe Gunze akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka (kulia) baada ya kumkabidhi zawadi walizoshinda kwenye Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Afrika yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka (wa pili kushoto) akiwa na wafanyakazi wa Mamlaka wakiwa na zawadi walizopata baada ya banda lao kushika nafasi ya kwanza katika kutoa huduma bora wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyomalizika hivi karibuni.

Na Francis Dande wa Blogu ya Jamii
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo wamekabidhiwa zawadi mbalimbali walizopata wakati wa Maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyomalizika hivi karibuni katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea zawadi hizo na kufanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi huyo aliwapongeza wafanyakazi hao kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoionyesha wakati wote wa Maonyesho hadi kuibuka washindi wa kwanza katika kipengele cha kutoa huduma bora pamoja na banda lao kushika nafasi ya pili kwa ubora.

‘Napenda kuwapongeza sana kwa kazi nzuri na heshima na sifa nzuri mliyoipatia Mamlaka yetu tunatambua juhudi zenu na muongeze jitiada katika kazi zenu za kila siku’ alisema Mkurugenzi huyo.

Naye Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Siylvia Lupembe Gunze alisema kuwa kujituma na kufanya kazi kwa pamoja ndio kulikowafanya kuibuka washindi katikaMaonyesho hayo yaliyozishirikisha nchi mbalimbali kutoka katika Ukanda wa Afrika.

Afisa Biashara wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Leila Kisinda na mfanyakazi mwenzake wakiteta jambo wakati wa zoezi la upandaji miti 600 kwenye Shule ya Msingi Msamvu B Morogoro lililowashirikisha walimu na wanafunzi wa shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti 21,000 iliyozinduliwa hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya shule ya Msingi Msamvu B, Nassoro Korwe akisisitiza jambo mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upandaji miti 600 iliyotolewa na Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro. Kushoto ni Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Morogoro, Bakari Hamis na kulia ni Meneja Muendeshaji wa benki hiyo Hogla Laiser.
Meneja wa benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Carlos Msigwa akimkabidhi mti Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Morogoro, Bakari Hamis wakati wa zoezi la upandati miti 600 kwa shule ya msingi Msamvu B kati ya 21,000 iliyotolewa na benki ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania Tawi la Morogoro akishirikiana na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Msamvu B iliyopo Morogoro mjini kuchota maji kwa ajili ya kumwagilia miti 600 waliyoipanda shuleni hapo ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya benki hiyo ya kupanda miti 21,000 iliyozinduliwa hivi karibuni Chanika jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Msamvu B, Mfanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania na Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Miti TSA Morogoro wakishiriki kupanda miti 600 kwenye shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti 21,000 iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni Chanika Msongola jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Katika kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya miti ya asili Benki ya KCB Tanzania Tawi la Morogoro imeitikia wito huo kwa kupanda miti 1,350 yenye thamani ya shilingi Milioni 3.5/-.

Miti hiyo imepandwa katika shule za Msingi Kiegea, Mibulasi na Msamvu B zote za mkoani Morogoro zoezi lililoendeshwa kwa ushirikiano wa Wafanyakazi wa benki hiyo, Walimu, Wajumbe wa kamati za shule, wanafunzi, wazazi na Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Morogoro, Bakari Hamis na Watendaji wa Wakala wa Mbegu za Miti TSA Morogoro.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upandaji miti, Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Carlos Msigwa amesema kuwa benki yake imejikita kwenye upandaji miti kutokana na baadhi ya watu kuona mazingira sio jambo la msingi kwao.

Msigwa amefafanua kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na kukua kwa shughuli za kibinadamu jamii isipopambana na kuidhibiti hali hiyo kwa kupanda miti na kuacha kuharibu maziungira jangwa na maafa vitazidi kutokea.

“Kupanda miti katika maeneo ya shule sio tu kunalinda mazingira, bali pia kunaepusha shule kuezuliwa mapaa na vimbunga ama upepo mkali. Vilevile wanafunzi mbali ya kujipatia matunda wanaweza kujipumzisha chini ya miti kwa ajili ya kujisomea,” alisema Meneja Msigwa.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya shule ya Msingi Msamvu B, Nassoro Korwe ameziomba taasisi zingine kuiga mfano huo kwa kuisaidia shule hiyo kukabiliana na changamoto zingine zinazojitokeza.

Akitaja baadhi ya changamoto Mjumbe Korwa amesema licha ya Benki ya KCB Tanzania kuwapandia miti wanakabiliwa na ukosefu wa maji kwa ajili ya kumwagilia miti hiyo ili isife kwa ukame.

“KCB Morogoro tayari wametupandia miti, tunaomba wahisani wengine wajitokeze kutusaidia upatikanaji wa maji kwa kipindi cha mwanzoni ili wanafunzi wayatumie kumwagilia miti. Hilo lisipofanyika mchango huu wa wahisani utakuwa umepotea bure.

Katika hatua nyingine Kiranja mkuu wa shule hiyo Hadija Maganga ameishukuru benki hiyo kwa msaada huo na kusema sasa watakuwa katika mazingira safi na salama kwa ajili yak masomo.

Mbali na hilo alitumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa benki hiyo kuangalia namna ya kuisaidia shule hiyo madawati ili kukabiliana na tatizo la baadhi ya wanafunzi kubanana ama kukaa kutokana na upungufu wa vifaa hivyo.

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget