HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 26, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bertha Mamuya (katikati) wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Rashid Abdallah wa IOGT wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.
Vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya, Rajab Huseein na Tatu Mapando, wakitoa ushuhuda kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kuacha kutumia madawa hayo.
Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.
Kikundi cha Sanaa cha Temeke, kikitoa burudani wakati wa sherehe hizo
Baadhi ya vijana waliowahi kutumia madawa ya kulevya wakipita na mabango mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yenye ujumbe wakitaka kusaidia dawa na Serikali dawa za kuzuia kutumia madawa, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakipita mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu suala zima la kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.
Bibi Kizee akipita mbele ya mabanda kukusanya vipeperushi katika kilelel cha maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya, "Hapa ujumbe utafika kwa wajukuu".
Baadhi ya Vijana wakiingia kwenye viwanja hivyo kwa maandamano ya staili ya kufanya mazoezi na kuimba.Picha na Muhidin Sufiani - OMR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad