Mtaa Kwa Mtaa Blog

Latest Post
1 AFRICANLYON AFYA AIRTANZANIA AJALI AJIRA ARUSHA ATCL AZAMFC BARABARA BEACH SOCCER BIASHARA BIASHARA. BU BUNGE BURUDANI BURUNDI CCM CONGOBR DAR ES SALAAM DARAJA LA KIGAMBONI DAWASCO DINI DODOMA EAC EID ELIMU EPL FEDHA NA UCHUMI FILAMU GAMBO GOFU H HABARI HABARI MCHANGANYIKO HABARI MICHEZO HABARI ZA BIASHARA HABARI ZA NYUMBANI HALI YA HEWA HARUSI HIFADHI HIFADHI. HISTORIA IBADA IKULU JAMII JESHI JESHI LA POLISI JK JKT-RUVU KAGERA KAGERA SUGER KAITABA KAMERA YA MTAA KWA MTAA KANDA YA ZIWA KARATE KARIAKOO KAZI KIFO KIGOMA KILIMANJARO KILIMO KIMATAIFA KITILYA KUMBUKUMBU KUOGELEA KUPATWA KA JUA KUPATWA KWA JUA KUTOKA BUNGENI LOWASSA LYON MAAJABU MADAWATI MADINI MAENDELEO MAFUNZO MAFUTA NA GESI MAGAZETI MAGEREZA MAHAFALI MAHAKAMA MAISHA MAJI MAJIMAJI MAKALA MAKAMU WA RAIS MAKONDA MALIASILI MAPATO MAREKANI MASUMBWI MATANGAZO MATUKIO MATUKIO MTAANI MAWASILIANO MAZINGIRA MBAOFC MBEYACITY MESSI MGAMBO MICHEZO MIFUGO MIFUKO YA JAMII MISS TZ MITINDO MIUNDOMBINU MOROGORO MSIBA MTAA KWA MTAA TV MTIBWA MUHAS MUZIKI MWANZA NANENANE NDONDO NHC NIDA NISHATI NYEREREDAY PICHA PPF RAIS MAGUFULI RATIBA RIADHA RUVU SADC SANAA BURUDANI SANAA NA UTAMADUNI SERENGETIBOYS SHEREHE SHERIA SIASA SIKUKUU SIMANZI SIMBASC SIMULIZI SOKA SONGWE TAHADHALI TANGA TANZIA TBL TEKNOLOGY TEKNOLOJIA TETEMEKO TRL TTCL TUZO UBUNIFU UCHAMBUZI UCHUKUZI UCHUMI UFARANSA UFUGAJI UGANDA UHURU DAY UJASILIAMALI UJENZI UK UKUTA ULAYA UMOJA WA TAIFA UREMBO USAFIRI USALAMA UTAFITI UTALII UTAMADUNI UTURUKI UWEKEZAJI VIJANA VIOJA VIWANDA VODACOM VPL WANAWAKE WAREMBO WASANII WATOTO WATU WAWAKILISHI WAZEE WAZIRI MKUU YANGA ZANZIBAR ZIMAMOTO

Rais wa Marekani Donald Trump amechukua hatua ya kwanza akiwa madarakani, kutia saini agizo lake la kutaka kufanyiwa mabadiliko ya sera ya matibabu ya rais aliyemaliza muda wake Barack Obama.

Agizo hilo la rais Trump, limeziagiza taasisi husika kuangalia namna ya kupunguza mzigo wa kiuchumi uliosababishwa na sheria ya matibabu, inayojulikana zaidi nchini humo kama Obamacare.

Akiapishwa jana rais Trump, aliahidi kuanzia jana kuwa ataweka maslahi ya Marekani kwanza, kufufua viwanda na kujenga miundombinu ya Marekani ambayo amesema imeoza na kutelekezwa.

Baadaye leo kundi la wanawake 200,000 wameahidi kushiriki maandamano ya Wanawake Jijini Washington, ambayo waandaji wamesema yanalenga kuangazia ubaguzi na suala la usawa ambalo linakabiliwa na tishio chini ya utawala wa Trump.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 2.4 kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji katika mji wa Makambako mkoani Njombe

Ametoa kauli hiyo siku ya Alhamisi, Januari 19, 2017 wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Polisi Makambako ulipofanyika mkutano wa hadhara akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.

Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi za salama katika umbali usiozidi mita 400 kama inavyosema sera ya maji.

Hata hivyo aliwataka wananchi kutofanya shughuli za kijamii katika vyanzo vya maji ili kuvilinda. Alisema Serikali inatumia fedha nyingi kutafuta maji kwa sababu vyanzo vingi zimekauka kutokana na shughuli za kibinadamu.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alizungumzia suala la madai ya fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa kituo cha ukaguzi cha pamoja na soko la kitamaifa katika eneo la Makambako aliahidi kuwa watalipwa.

“Fidia zenu mtalipwa hivi katibuni baada ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kukamilisha taratibu za ulipaji,” alisema. Wananchi hao walilalamikia ucheleweshwaji wa malipo ya fidia hizo kupitia katika mabango mbalimbali pamoja na mbunge wa Njombe, Mheshimiwa Deo Sanga.

Serikali imeanzisha eneo la Idofi lililoko Makambako kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari ya mizigo ili kupunguza vikwazo vya kibiashara barabarani kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kituo hicho kitakuwa na vituo vidogo vya Polisi, Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Maliasili pamoja na vituo vya mizani.

Awali mbunge wa jimbo la Njombe Mheshimiwa Sanga alisema moja ya changamoto inayowakabili wakazi wa mji wa Makambako ni ucheleweshwaji wa malipo ya fidia kwa waliopisha ujenzi wa kituo hicho hali inayosababisha baadhi yao kwenda kudai fidia hiyo kwake.

”Mheshimiwa Waziri Mkuu leo na sisi wananchi wa Makambako tutapona. Baba Majaliwa hawa wananchi wanadai fidia yao kwa muda mrefu na baadhi yao wamefikia hatua ya kuja kulala nje ya nyumba yangu wakigoma kuondoka hadi niwape ufafanuzi wa malipo yao,” alisema.

Mbali na kuwasilisha changamoto hiyo mbunge huyo pia aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada zake za kuboresha maendeleo ya wananchi hususan wakazi wa jimbo la Njombe.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe, Bw. Christopher Ole Sendeka alisema Serikali imetenga sh. bilioni 2.8 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la chuma lenye urefu wa mita 95 katika mto Ruhuhu.

Alisema mkataba wa ujenzi wa nguzo za daraja tayari umesainiwa kati ya mkandarasi wa kampuni ya M/s Lukolo na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa gharama ya sh bilioni 6.17 na muda wa utekelezaji ni miezi 24.

Akizungumzia mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi Bw. Ole Sendeka alisema mkoa unaendelea na kampeni za upimaji, zilizowezesha watu kufahamu afya zao na kuchukua tahadhari ya jinsi ya kujikinga na kuepuka maambukizi mapya.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 20, 2017.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akisalimiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni wakati alipotembelewa ofisini kwake leo 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifanya mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni kuhusu mausuala mbalimbali ya habari ofisini kwake 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifafanua baadhi ya masuala mbalimbali yanayohusiana na habari wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni ofisini kwake 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) akieleza masuala mbalimbali yanayohusiana na habari na utamaduni wa Italia wakati alipomtembelea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye leo 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.


Ijumaa Januari 20,2017 kumefanyika mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu umefanyika katika ukumbi wa mikutano Karena Hotel Mjini Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wa kitaifa wa CHADEMA wamehudhuria mkutano huo ambao umeenda sambamba na kufanya uchaguzi wa viongozi wa kanda ya Serengeti ambapo John Heche amechaguliwa kuwa mwenyekiti,Gimbi Masaba kuwa makamu mwenyekiti n Catherine Ruge kuwa mweka hazina.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe ametumia mkutano hiyo kutoa ujumbe kwa taifa kupitia vyombo vya habari.
Mbowe amesema nchi ya Tanzania inapitia changamoto nyingi kwa kipindi hiki lakini kubwa zaidi kuliko yote ni hofu inayotamalaki ndani ya taifa kwamba watu wameanza kujiona kuwa hawako salama sana ndani ya nchi yao.
Amesema kuna watu ambao wana hofu ya njaa,hofu ya kuporomoka kwa uchumi,hofu za kiusalama,lakini CHADEMA ina hofu kubwa kuhusu usalama wa viongozi wake,hofu kubwa kuhusu kutokutendewa haki viongozi wa cha hicho kuanzia viongozi wa kitaifa,kwenda kwa wabunge,madiwani,wenyeviti wa vijiji,wenyeviti wa mitaa hata na vitongoji pamoja na wanachama wao.
“Badala ya kujengwa hofu ni lazima sasa tusimamie imara kuijenga CHADEMA yenye nguvu kujenga upinzani wenye nguvu,kusimama kwa haki bila kuogopa”,amesema Mbowe.
“Ni juzi tu rais amemteua wabunge wengine katika orodha ya wabunge 10 anaoweza kuwateua,katiba ya nchi inasema anapaswa ateue 10,lakini kati yao wasipungue wanawake watano,lakini hadi jana rais ameshateua wabunge nane kati yao sita ni wanaume kwa maana hiyo tayari ameshavunja katiba”,anasema Mbowe.
   
Kushoto ni mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman  Mbowe,katikati ni katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji na naibu katibu mkuu Chadema bara John Mnyika wakiteta jambo wakati wa mkutano maalum wa Chadema kanda ya Serengeti uliofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Wa kwanza kushoto ni Makamu mwenyekiti Chadema taifa Zanzibar,Said Issa Mohammed.Wa kwanza kulia ni naibu katibu mkuu Chadema taifa Zanzibar Salum Mwalim
Viongozi mbalimbali wa Chadema taifa wakiwa ukumbini
Viongozi wa Chadema wakiwa ukumbini
Viongozi wa Chadema wakiwa meza kuu
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini
Katibu mkuu wa Chadema taifa Vicent Mashinji akizungumza ukumbini ambapo alisema vitendo mbalimbali wanavyofanyiwa viongozi wa chama hicho ni ishara kubwa kuwa ushindi wa chama hicho umekaribia
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa ukumbini
Katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji akizungumza
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akitoa ujumbe kwa taifa kuhusu hali ya nchi ya Tanzania hivi sasa
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akizungumza ukumbini.Waliokaa kushoto ni wagombea katika uchaguzi wa viongozi Chadema kanda ya Serengeti 
Katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji akisoma katiba ya nchi.
Wajumbe wa mkutano wakimsikiliza mwenyekiti wao
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akisisitiza jambo
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Donald Trump ameapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani. Trump amechukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama saa mbili usiku kwa muda wa Afrika Mashariki. Wafuasi wake walikusanyika kwa wingi barabara za Washington.
Donald Trump amekuwa rais wa 45 wa Marekani amerejelea ahadi yake ya kampeni ya kuifanya nchi yake kuwa taifa lenye nguvu zaidi kuliko hapo awali, Hata hivyo maelfu waandamana nchini Marekani kupinga kuapishwa kwake.

Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump pamoja na familia yake wakifurahia mara baada ya kumaliza kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani,
Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump akihutubia taifa kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Taifa hilo.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wanashuhudia kuapishwa kwa Donald Trump
Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump(mwenye tai nyekundu) akimsindikiza rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na aliyekuwa Makamu wa rais wake 
Rais wa Marekani, Donald Trump akipeana mkono na rais aliyemaliza muda wake Barack Obama 

 Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama akiwapungia mkono 
Herikopta  iliyombeba rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na mke wake ikiondoka 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Dkt. Emanuel Nchimbi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazili, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. James Msekela  kuwa Balozi wa Tanzania Geneva –Umoja wa Mataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Mbelwa Kairuki kuwa Balozi wa Tanzania nchini China, Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. George Madafa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Elizabeth Kiondo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Fatma Rajab  kuwa balozi wa Tanzania nchini Qatar, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza machache baada ya kuwaapisha mabalozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017. Picha na IKULU

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mabewani mjini Makete, januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Ujuni wilayani Makete walioziba barabara wakitaka asimame kuwasalimia Januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ndama waliokuwa wakinyweshwa maziwa wakati alipotembelea shamba la ng’ombe la Kitulu wialayani Makete Januari 20, 2017. 


 Msemaji wa Jeshi la polisi,Advera Bulimba akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  wananchi kuwa makini pindi wanapofanya biashara kwa njia ya mitandao kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakiibiwa kwa kutokuchukua tahadhari za kutosha,leo jijini Dar es Salaam.

Na Emmanuel Masaka, Globu Jamii.
JESHI la polisi limewataka wafanya biashara kuhakikisha kuwa  wanaomba ulinzi kutoka jeshi la polisi au makampuni binafsi ya ulinzi yanayo husika na kusafirisha fedha ilikupunguza matukio ya kuvamiwa na kuibiwa fedha wanapokuwa wakisafirisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es salaam Msemaji wa Jeshi la polisi Advera Bulimba   amesema uchunguzi wa Jeshi la polisi umebaini kuwa uhalifu huo umekuwa ukisababishwa na wafanya biashara husika kutokuwa na usiri pamoja na kutokuomba ulinzi kutoka Jeshi la polisi au makampuni binafsi ya ulinzi yanayoshughulika na kusafirisha fedha.

‘’Jeshi la polisi nchini  linatoa wito kwa wafanya biashara kuhakikisha kuwa wanaomba ulinzi kutoka jeshi la polisi aumakampuni binafsi ya ulinzi yanayoshughulika na kusafirisha fedha pia  wasafirishaji wa fedha kuwa na usiri katika michakato yote inayohusiana   na usafirishaji wa fedha ilikuweza kupunguza matukio ya hayo’’ amesema Advera. 

Aidha Msemaji huyo amesisisitiza kuwa  wananchi kuwa makini pindi wanapofanya biashara kwa njia ya mitandao kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakiibiwa kwa kutokuchukua tahadhari za kutosha kabla  ya kutuma fedha.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Jeshi la polisi,Advera Bulimba leo jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wadau wa Baraza la Baraza la Wakunga hawapo pichani wakati wa kuzindua mradi wa Mkunga Okoa Maisha kwa kushirikiana na watu wa Canada.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kuzindua  mradi wa Mkunga Okoa Maisha , wa kwanza kushoto ni Balozi wa Canada  Bi. Susan Steffan na wakawnza kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo kwa viongozi wote nchini kuacha mara moja kuwakamata wauguzi,  wakunga na kuwaweka ndani na badala yake wanapaswa kufuata taratibu zilizopo.
Akizungumza  hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu  alisema wakunga wanalo baraza ambako ndilo suluhishi la matatizo yao.
"Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa pale ambapo muuguzi au mkunga anapokosea  zipo taratibu za kufuata na siyo kumweka ndani kwani kuna Baraza la Wakunga ambalo lina Mamlaka ya kisheria za kuchukua kwa mkunga yoyote ambaye amekwenda kinyume.
"Tunao Wakunga na wauguzi ambao wanafanya kazi zaidi ya masaa, tumeona kilichotokea Sikonge, kiongozi anakuja juu kwanini mtoto amepewa dawa ya Quinn," alisema Ummy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari amesema kuwa mradi huo unalenga  kupunguza vifo katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu hivyo wauguzi na wakunga ni vema wakashirikiana na Baraza hilo ili kufanikisha malengo yao.

  Kaimu Mkuu wa Idara ya Miradi ya Ujenzi kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi  Injinia Wambura M. Wambura akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu jukumu la ukaguzi wa kiufundi au kitaalam wa miradi ya ujenzi nchini jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo) 
Kaimu Mkuu wa Idara ya Majengo kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi Injinia Kissamo Fredrick akiongea na wanahabari kuhusu mafanikio ya Baraza hilo katika utekelezaji wa jukumu la kufanya ukaguzi wa kiufundi jijini Dar es Salaam leo.
SERIKALI kupita Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) imefanya ukaguzi wa miradi mikubwa 163 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2 ikijumuisha Barabara, majengo, maji na viwanja vya ndege.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu wa Idara ya Uhandisi  wa Baraza hilo Mhandisi Wambura M. Wambura alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya ukaguzi huo.
Mhandisi Wambura amesema kuwa miradi  yote iliyofanyiwa ukaguzi inatekelezwa chini ya ufadhili wa Serikali.
“Shughuli za kiukaguzi zilizofanyika ni pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya michakato ya manunuzi, utekelezaji wa mikataba, utekelezaji wa miradi,ongezeko la gharama za miradi, pamoja na ubora wa kazi zilizofanyika,” alisisitiza Mhandisi Wambura.
Aliongeza kuwa lengo la kaguzi hizo ni kuhakikisha kuwa thamani ya fedha inalingana na ubora wa miundombinu iliyojengwa katika eneo husika.
Aidha, Mhandisi Wambura amesema kuwa katika kipindi cha 2015/2016 baraza lilifanya ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya matengenezo ya barabara kwa halmashauri zote za Wilaya pamoja na TANROADS kwa Mikoa ya Mbeya,Songwe,Rukwa,Katavi,Kigoma, na Shinyanga ambapo miradi hiyo iliyotekelezwa kwa fedha za mfuko wa Barabara.
Miradi mingine iliyofanyiwa ukaguzi wa kiufundi  mwaka 2011 ni 14 iliyohusu  ujenzi wa vituo vya afya na 36 ya ujenzi wa zahanati 50 iliyotekelezwa kwenye Halmashauri za Wilaya 20.
Akizungumzia changamoto zilizobainika katika ukaguzi unaofanywa na Baraza hilo Wambura alibainisha kuwa ni kutozingatiwa kwa taratibu za kusimamia ubora wa kazi na maandalizi hafifu ya miradi katika hatua za mwanzo katika utengaji bajeti yakutosha,usanifu na ukadiriaji gharama za ujenzi.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya majengo Bw. Kissamo Elias alitoa wito kwa wadau wa sekta hiyo kulitumia Baraza hilo kufanya kaguzi katika miradi wanayotekeleza ili kuongeza tija hali itakayochochea ukuaji wa sekta hiyo.
Baraza la Taifa la Ujenzi ni kitovu cha uratibu wa sekta ya ujenzi kwa taasisi zote zinazoshughulika na shughuli za ujenzi pamoja na wadau ili kuleta umoja,uwiano, na ushirikiano katika utendaji ndani ya sekta ya ujenzi,Baraza linaendelea kusimamia na kuongoza juhudi za kukuza na kuendeleza sekta ya ujenzi nchini.
Baraza la Taifa la Ujenzi ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge namba 20 ya mwaka 1979 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008,baraza lipo chini ya Wizara ya ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget