HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 17, 2017

MFAHAMU MISS TANGA 2001 ALIYEJIKITA KATIKA KUSAIDIA JAMII

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMA Mwanamke ukiamua kujitoa na kupigania nini unafanya lazima utafanikiwa, nami naweza kusema kufika kwangu ni pale nilipoamua kujituma, kujiamini na kutambua nini malengo yangu.

Hayo ni baadhi ya maneno aliyotoa mwanamke mjasiriamali Sophia Khalid Byanaku, ambaye ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Doctor's Plaza, alikuwa akizungumza na Globu hii. 

Sophia Khalid Byanaku  ni mke wa Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), ana Elimu ya Shahada ya sosholojia (Degree in Sociology), Shahada ya uzamili Sera za afya Mipango na Usimamizi (Master in Health Policy Planning and Management.

Ulianzia wapi,


Byanaku : Mwaka 2001 nilishiriki mashindano ya urembo kwa mkoa wa Tanga na kufanikiwa kuchukua taji la Miss Tanga 2001 na kupata nafasi ya kuwa katika kumi bora ya Miss Tanzania ambapo taji lilichukuliwa na mrembo Millen Hapiness Magese. 

Unajivunia nn kupitia Miss Tanzania,
Byanaku: Najivunia mambo mengi kupitia ushiriki wa Miss Tanzania mwaka ule kwani umeweza kunipa ujasiri wa kuweza kupambana kwa namna nyingine na hata miaka yetu tuliweza kupata nafasi nyingi za kushiriki kijamii zaidi.

Baada ya kumalizika kwa Miss Tanzania ulijikita wapi zaidi:
Byanaku:  Kabla ya kufungua Kliniki ya Doctor's Plaza, nilikuwa mfanyakazi wa benki Stanbic Bank Tanzania kwa takribani miaka 6, baadae nikafanya kazi benki ya NMB kwa muda wa mwaka mmoja na African Life Assurance (Sanlam).

Doctors Klinik ilianza lini?

Byanaku: Rasmi mwaka 2012 kwa kituo kimoja wakiwa wamejikita katika kutibu magonjwa ya moyo tu lakini sasa wanatoa matibabu ya ya magonjwa mbalimbali ya binaadamu na tayari wana vituo  vitatu ambavyo vyote vipo jijini Dar es Saalam.

Madhumuni ya kufungua Doctors Kliniki ni nini?
Byanaku: Lengo kuu la kufungua vituo hivyo ni kwa sababu napenda sana kujishughulisha na jamii, hivyo kuwa na vituo hivyo amejua mambo mengi kuhusu jamii inayomzunguka. 

Matarajio ya Byanaku ya baadae:
Byanaku:  Matarajio yangu ya  baadae ni kuwa na Hospitali kubwa ya kisasa Tanzania ambayo itaweza kutoa huduma karibia zote kwa wahitaji,na pia nataka kuwa Mtaalam wa Health care Management kwa Tanzania,yani nataka kukiwa na uhitaji wa ushauri kuhusu masuala ya uongozi wa Afya Tanzania mimi niwe mtu wa kwanza kufikiria kusaidia.

Changamoto anazozipata katika vituo  Doctor's Plaza
Byanaku: Kuna changamoto mbalimbali zinazotukabili kwenye vituo vyetu vya Doctor's Plaza ila kikubwa zaidi  ni madaktari kwani ni wachache ambapo mpaka sasa tuna madaktari 32 kutoka Muhimbili ila tunaendelea kufanya jitihada kuhakikisha  watu wanapata huduma wanazohitaji za matibabu. 



Anachojivunia kama mwanamke mjasiriamali:

Byanaku: Naweza kusema katika kufanikisha jambo uliloamua kulifanya, kwenye hili hakuna mwanaume wala mwanamke ili kuweza kufikia mafanikio yoyote,lazima kufanya kazi kwa bidii na kujituma,na sio kwa bidii tu lakini pia kwa akili,kusimamia malengo yako na pia kutokukubali kukatishwa tamaa na mtu yoyote yule,ilhali huvunji heshima ya mtu.
Wanawake tusiogope wala kuona aibu fursa zinapotokea tuzikimbilie bila aibu wala woga na tuonyeshe uwezo wetu, kwa kusema haya haya Mimi mwenyewe bado sijafikia malengo yangu lakini nashukuru nimeweza kufikia kidogo safari bado ni ndefu tunajifunza kila siku na nina amini nitafika.
Unapaswa kujiwekea malengo na kuyafanyia kazi ili kuyafikia, kila unachoona kinaweza kufanyika na kufanikiwa kwa asilimia kubwa. 

Byanaku nje ya kazi ni nani?

Byanaku: Sophia Khalid Byanaku ni Mama wa watoto wawili, Nayla (6) na Akim(4), na nimeolewa na Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), muda wangu mwingi napokuwa nyumbani napenda kukaa na familia yangu.
Kama Mwanamke mara nyingi nakuwa na suluhisho na nafanikiwa kujigawa kwa usawa katika majukumu yangu ya nyumbani, napenda sana kuwa na familia pale ninapoukuwa nyumbani  bila kuchanganya yote haya nayafanya na naweza ndiyo maana natarajia kuongeza zaidi hapa nilipoanza, kikubwa mwanamke unaweza kufanikiwa kama kweli umeamua kulifanya lako katika kuleta maendeleo katika jamii hasa iliyokuzunguka

Anasema hata hivyo bado anajitahidi kuwa nkujifunza kwa kusoma vitabu na hata kuuliza watu walionitangulia waliwezaje na kufanikiwa, lakini pia kuweza kufanikiwa haya ni lazima pia upate ushirikiano kutoka kwa familia,ambayo nashukuru ninapata ushirikiano.

Unapendelea nini? 

Byanaku: Ni mpenzi wa kusoma vitabu Sana kwa sasa nasoma vitabu viwili; My Personal MBA By Josh Kaufman na The E Myth Revisited By Michael Gerber na kitabu ninachotarajia kusoma ni The Miracle Morning by Hall Elroy. Napenda Kusafiri,Mziki,na kusoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad