Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nzega, Peter Mashili amesema kuwa ameamua Kugombea Ubunge kwa sababu wananchi wa Nzega wanahitaji nguvu na kasi Mpya ili kuendeleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025-2030.
Amesema akiteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kwenye mchakato wa kura za maoni na baadaye akiteuliwa kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Nzega Mjini atajikita zaidi katika ushirikishwaji wa wananchi kwenye mambo ya msingi ya maendeleo endelevu, kuwasemea wananchi Changamoto zinaowakabili, kuwapambania ili wanufaike na Fursa zinazotolewa na Serikali hasa katika uendelevu wa sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kwa lengo la Kukuza kipato kwa wananchi ili wajiendeleze kiuchumi na kukuza pato la Taifa.
Peter Mashili ambaye ni mbobezi katika uchimbaji na uuzaji wa madini ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mbugani katika Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ni miongoni mwa wafanyabiashara mahiri kuwahi kutokea nchini Tanzania ambao wana historia kubwa katika ushiriki wa shughuli za kijamii hususani uboreshaji wa miundombinu ya elimu.
Lakini wadadisi wa masuala ya kisiasa katika Jimbo la Nzega wanasema MASHILI wakati wake umefika sasa wa kugombea ubunge wa Jimbo hilo kutokana na kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wa wilaya ya Nzega kwa miaka mingi iliyopita na hadi Sasa bado anaendelea kufanya hivyo.





No comments:
Post a Comment