HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 27, 2011

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KUPITIA BIA YA BALIMI EXTRA LAGER-KAGERA

Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Ngoma za Asili Mkoani Kagera,Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba,Mh. Ndyamukama akihutubia washiriki wa Mashindano ya Ngoma za Asili yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Balimi Extra lager, kushoto ni Andrew Mbwambo Meneja Mauzo na Erick Mwayela, Meneja Matukio kanda ya ziwa.
Mshindi wa kwanza Mashindano ya Ngoma za Asili kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba aliepokea fedha taslim laki tano (500,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Ndyamukama akisalimiana na Andrew Mbwambo Meneja Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania. Mshindi wa pili katika mashindano hayo kilikuwa ni kikundi cha Rugu toka Karagwe walijipatia laki Nne(400,000/=), wa tatu ni Kabale toka Manispaa ya Bukoba walijipatia laki tatu(300,000/=).
Kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza.
Kundi la Rumanyika kutoka Karagwe wakionyesha umahiri wao wa ngoma za asili.
Hivi ndivyo mambo yalivyokua katika viwanja vya Kaitaba katika kumsaka mshindi wa mashindano ya ngoma za asili kupitia kinywaji cha Balimi Extra lager.


Makundi mbalimbali yakionyesha umahiri wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad