Timu shiriki katika mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa wavu zikifanya maandamano ya ufunguzi wa mashindano hayo ,maandamano yalianzia ofisi za Vodacom hadi uwanja wa Hindu Mandal.
Timu shiriki zikiwa zimejipanga tayari kwa ufunguzi wa mashindano ya klabu bingwa Tanzania.
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa wavu nchini (TAVA)Augustino Israel Agapa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya klabu bingwa yanayo fanyika mjini Moshi ,Jumla ya timu sita kutoka mikoa mbalimbali zinashiriki mashindano hayo.Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wakiwa ndio wadhamini wakuu wa mashindano walikuwepokushuhudia ufunguzi,shoto ni meneja mauzo mkoa wa Kilimanjaro Kizumo Kizango na Emanuel Carl ambaye ni mwakilishi mauzo mkoa wa Kilimanjaro,kulia ni katibu wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Kilimanjaro Alfred Serengia. 
Meneja mauzo wa Vodacom mkoa wa Kilimanjaro,Kazumo Kizango akizungumza wakati wa ufunguzi huo.



Mambo Michuzi Mdogo Junior,
ReplyDeleteHuyo anayeongea sio Kizumo Kizango, Kizumo Kizango ni huyo aliyekaa mwenye shati jeupe.