HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 16, 2010

Kampuni Ya RBP Oil & Industrial Technology Ltd Yaadhimisha Siku Ya Mtoto Wa Afrika na Watoto Yatima Leo

Rais wa RBP OIL& Industrial Technology Ltd,Mama Rahma Al Kharoos akiongea leo na waandishi wa Habari waliofika katika hotel ya South Beach,Kigamboni.Mama Rahma leo ameweza kuwakutanisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu toka katika vituo 6 vinavyolea watoto hao pamoja na timu ya Taifa ya wanawake (TWIGA STARS) kwa kuweza kula nao pamoja chakula cha mchana na watoto hao ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika,vituo hivyo ni NEW LIFE,HANANASIFU,UMRA,TANZANIA MITINDO HOUSE,MOTHER TERESA pamoja na CHACHUMA.Nahodha wa timu ya Twiga Stars,Sophia Mwasikile akitoa shukrani zake za dhati kwa niaba ya Timu hiyo kwa Rais wa RBP OIL& Industrial Technology Ltd,Mama Rahma Al Kharoos kwa kuwaandalia hafla hiyo siku ya leo.
Meneja uhusiano wa kampuni ya RBP OIL& Industrial Technology Ltd,Ibrahim Khatrush akiwa pamoja na Afisa kutika Ustawi wa Jamii,Bi. Sophia Ally wakipanga namna watakavyogawa tisheti kwa watoto ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika inayoadhimishwa tarehe kama ya leo kwa kila mwaka katika hotel ya South Beach leo.
watoto wakipata chakula cha mchana katika hotel ya South Beach,Kigamboni leo.
wadau wakiulizia chachandu kama inapatikana kwa muhudumu wa hotel hiyo ya South Beach.
baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) wakiwachukulia chakula watoto waishio katika mazingira magumu.
watoto wakiogelea kwa furaha
Fide na Martin wakiperuzi
wadau wa habari toka shoto ni Dinah Zubeir wa Tanzania Daima,Vicky Kimaro wa Mwananchi pamoja na Angel Msangi wa TBC wakiwajibika leo.
Rais wa RBP OIL& Industrial Technology Ltd,Mama Rahma Al Kharoos akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Twiga Stars.
Rais RBP OIL& Industrial Technology Ltdakiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio katika mazingira magumu toka vituo mbali mbali pamoja na timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad