Dodoma, Julai 25, 2025
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bi. Sakina Mwinyimkuu, amewataka watumishi wa umma kutumia maarifa waliyopata katika mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika kazi zao.
Akifunga rasmi mafunzo hayo ya siku tano yaliyofanyika jijini Dodoma, Bi. Sakina amesisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa kazi bora unaozingatia matokeo (results-based performance), kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Mafunzo haya si kwa manufaa yenu binafsi pekee, bali yatumike kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya katika taasisi zenu, sambamba na kuendeleza maadili ya uwajibikaji,” amesema Bi. Sakina.
Ametoa rai kwa washiriki kuwa mabalozi wa kueneza uelewa huo kwa wengine katika maeneo yao ya kazi, ili kuimarisha utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia viwango vya kitaifa vya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo.
Friday, July 25, 2025

Home
Unlabelled
BI. SAKINA MWINYIMKUU: JENGENI UTAMADUNI WA UTENDAJI UNAOTEGEMEA MATOKEO
BI. SAKINA MWINYIMKUU: JENGENI UTAMADUNI WA UTENDAJI UNAOTEGEMEA MATOKEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment