VIPINDI vya mashindano ya Miss Universe Tanzania 2025 vinatarajia kuanza kuonekana kuanzia leo Julai 25 mwaka huu katika king’amuzi cha Startimes Tanzania kupitia Chaneli yake ya ST Swahili lengo likiwa kuwapa nafasi Watanzania kuona matukio mbalimbali katika Miss Universe nchini.
Akizungumza leo Julai 2025 jijini Dar es Salaam ,Mkurugenzi wa Kampuni ya MILLEN PRIVÉ & Co. LIFESTYLE Bespoke Luxury Lifestyle & Hospitality Management ambaye pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness Magese amesema kuanzia leo wanatangaza rasmi kuwa kutakuwa na kipindi cha urembo kupitia Miss Universe Tanzania.
“Watu wamekuwa wakiona warembo wanaingia kambini ,wanatoka kambini,hivyo unakuwa haujui wanakuaje pale kambini,wamechaguliwaje.Kwahiyo mwaka huu kwa mara ya kwanza mtaona jinsi tulivyowachagua,tulivyowafundisha wakaiva mpaka siku ya mwisho.
“Katika Miss Universe Tanzania tumeshakwe da Arusha,Mwanza ,Dodoma ,Mbeya na Zanzibar na Kwa sasa hivi tuko Dar es Salaam.Hivyo mtaona jinsi ambavyo tumepata wasichana tofauti tofauti na kuanzia hapo onesho la Miss Universe kupitia vipindi vitakavyoonekana Startimes Tanzania,” amesema Millen.
Mbali na kutangaza kuanza kurushwa kwa vipindi vya Miss Universe Tanzania 2025,ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Taifa lake la Tanzania, Watanzania wote kwa ujumla na wazazi wanaowalea wasichana ambao wamempa nafasi ya kumuamini na kuruhusu mabinti zao kufika katika mashindano ya Miss Universe.
“Tumeshapita katika Mkoa wa Arusha, Mwanza, Dodoma,Mbeya na kwa mara ya kwanza katika historia ya urembo tumeenda Zanzibar na kwa kipekee niishukuru Serikali ya Zanzibar kwa kunipa nafasi ya kuleta urembo kwasababu urembo huu ni wa kumuwezesha mwanamke na si kumdhalilisha au kumuharibia mambo makubwa ya mila na desturi.
“Miss Universe ni jukwaa kubwa sana duniani ambalo limejikita kumuwezesha mtoto wa kike au mwanamke na haijalishi ilimradi amefika miaka 18 ,awe ameolewa, hajaolewa ,awe na mtoto au hana hana,awe mrefu au mfupi,mwembamba au mnene wote wameruhusiwa kuja katika jukwaa la Miss Unirves.”
Ameongeza kuwa kwao upande wao wanaamini mwanamke akipewa nafasi ya pili anaweza kutimiza ndoto zao na kusisitiza amefurahi kuona mabinti wengi wamejitokeza Miss Universe.
Kwa upande wake Judith Ngussa ambaye ni Miss Universe Tanzania 2024 ametumia nafasi hiyo kuwashukuru mabinti wote waliojitokeza kwenye maonesho ya Miss Universe katika mikoa yote waliyopita.
“Tunawashukuru wazazi kwa kuwaruhusu mabinti zao lakini na wao wenyewe kwa juhudi zao na kuiamini kampuni ya dada yetu Millen ambaye amewekeza kwa ajili ya kuwawezesha mabinti wa Tanzania kupitia Jukwaa la Miss Universe.Hivyo naiomba Serikali kujitokeza na kutuunga mkono katika uwekezaji wa Miss Universe.
Wakati huo huo David Malisa ambaye Mkurugenzi wa Vipindi na Maudhui kutoka Kampuni ya Startimes Tanzania amesema wanayo furaha kukutana katika meza ya Miss Universe ambayo ni ya mapinduzi katika tasnia ya urembo ,hivyo ameipongeza Millen Privee ,na majaji wengine wote ambao wamezunguka katika mikoa mitano na leo wanamalizia Mkoa wa Dar es Salaam ambao unakuwa Mkoa wa sita.
“Kwahiyo haya yote ambayo yamefanyika mkoani watu walikuwa wanaona katika mitandao ya kijamii na hakuna anayejua nani amepita,ilikuaje ,kuna vitu vingi sana ambavyo vimetokea huko mkoani ambako tumepita na mojawapo ni stori kubwa za warembo jinsi walivyokuwa wanavutiwa na Millen mwenyewe.
“Leo tunatangaza hapa Miss Universe Tanzania 2025 vipindi vyake vitaonekana Startimes kupitia chaneli ya Startimes Swahili ambayo inapatikana katika king'ang'umuzi cha Star times pekee na vitakuwa vinaruka kila siku saa mbili na nusu usiku.
“Na tuliangalia kwanini tumeweka kwenye Startimes Swahili ni kwasababu kila mtanzania apate nafasi ya kuangalia kwasababu iko kwenye vifurushi vyote kabisa kuanzia kile cha bei ya chini ,unaweza kulipia kwa siku,wiki ,mwezi na bado ukaipata.Vipindi vitaoneshwa mpaka siku ya fainali ya Miss Universe Agosti 23 mwaka huu.”









No comments:
Post a Comment