HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 20, 2023

WAREMBO 20 MISS TANZANIA WAPAGAWA KISA MERCEDES BENZ

 


Zawaradi rasmi ya Miss Tanzania 2023 gari aina ya Mercedes benz yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 za Kitanzania ambapo Julai 22,2023 katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam kati ya washiriki 20 mmojawapo ataondoka na  gari hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Azama Mashango akiwapongeza wadau mbalimbali wanaoendelea kutoa ushirikiano katika shindano la Miss Tanzania na kuhakikisha shindano hilo linaendelea kwa lengo la kutimiza ndoto za wasichana wengi kwenye tasnia ya urembo huku akiwataka wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi Julai 22,2023 katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam kushuhudia Fainali ya Miss Tanzania 2023.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes ambao ndio Wadhamini wa Shindano la Miss Tanzania 2023 David Malisa akizungumza na Wanahabari Leo Julai 19,2023 kutangaza rasmi zawadi ya Miss Tanzania 2023 gari aina ya Mercedes benz yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 za kitanzania ambapo Fainali hiyo inatarajiwa kufanyika Julai 22,2023 katika Ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam
Meneja Mradi wa Shindano la Miss Tanzania 2023 Ombeni Phiri akifafanua zaidi kuwa washiriki 20 wameweza kujifunza vitu mbalimbali kambini kwa takribani siku 27 na hatimae Julai 22,2023 kufikia tamati

Na.Khadija Seif, Michuziblog
WAREMBO 20 wabaki vinywa wazi mara baada ya kutangazwa rasmi zawadi ya Miss Tanzania gari aina ya Mercedes benz yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 za Kitanzania pamoja na pesa taslim Milioni 10 kwa atakaeibuka Mshindi Usiku wa Julai 22,2023 katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Wanahabari wakati wa kutambulisha zawadi hiyo Leo Julai 19,2023 Jijini Dar es salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema kuwa Fainali ya Miss Tanzania itapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa warembo wenyewe huku akisisitiza kuwa Fainali hiyo itakuwa ya kitofauti kutokana na kupangika kwa matukio ya kiburudani zaidi.

"Nilipata nafasi ya kupita kambini kushuhudia mazoezi ya Fainali ya Miss Tanzania kutoka kwa washiriki wenyewe Kiukweli kuna hatari watu wanajifua namna ya kutembea jukwaani (catwalk) zaidi ya Mrembo Halima Kopwe (Miss Tanzania 2021) lipieni ving'amuzi mshuhudie burudani hiyo kupitia chaneli ya st bongo ndani ya Startimes. "

Malisa amewasihi watazamaji kulipia mapema ving'amuzi vyao ili kutazama mubashara Fainali hizo kwa wale ambao hawatabahatika kufika katika ukumbi wa the Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.

Nae Meneja Mradi wa shindano hilo Ombeni Phiri amesema Washiriki hao 20 kutoka kanda mbalimbali wanaenda kugombania gari hiyo ambapo ni kwa mara ya pili mfululizo gari aina ya Mercedes benz kutolewa kwa mshindi.

"Warembo 20 wamekuwa kambi kwa siku 27 na kujifunza vitu mbalimbali hivyo sio jambo rahisi kwa warembo hao kuwa sehemu moja kutokana na kila mshiriki ana tabia yake.''

Hata hivyo Phiri amewatakia kila la heri warembo hao 20 kuelekea fainali hiyo ambapo mmojawapo anaenda kubadilisha maisha yake kupitia tasnia ya urembo na mitindo.

Hata hivyo kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Azam Mashango amesema washiriki wote 20 watapewa fedha kama kiinua mgongo isipokuwa Mshindi wa nne,tano na sita watapewa Milioni 1 ,Mshindi wa 3 milioni 2 huku Mshindi wa pili akipatiwa Milioni 2 na wa kwanza milioni 10 huku Mshindi wa 6 hadi 20 wakiambulia laki 2 kila mmoja.

Mashango amewapongeza wadau mbalimbali wa shindano hilo wakiwemo Robby One pharmacy, Startimes na wengine kuhakikisha shindano hilo linafanyika na linaonyeshwa mubashara kwenye King'amuzi hicho ili kuwapa nafasi wadau wa urembo kuwaona wasichana hao wadogo wenye kiu ya kutimiza ndoto zao kupitia tasnia ya urembo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad