Njombe
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Philip Mpango amesema amekataa kupanda ndege na kuutumia usafiri wa barabara ili kuona changamoto mbali mbali ikiwemo za barabara na kufanyiwa kazi.
Dkt,Mpango ameeleza hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Makambako alipokuwa akielekea mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya ziara ya kikazi.
"Watu wangu walijaribu kunishawishi niende kwa ndege nikawaambia sisi hatutawali hayo mawingu nataka kupita watu wangu waliko,kwa kweli moja ya sababu zangu za msingi ni kuona barabara hii (Makambako - Songea) bahati nzuri naibu waziri ametoa maelezo kwa hiyo ninataka kusisitiza vipande vyote ambavyo vimewekewa fedha kwenye bajeti ya mwaka huu muanze kufanya kazi mara moja,kwa hiyo Lutukila - Songea nakwenda huko KM 98 kabla ya mwisho wa mwaka nisipokuta hatua tutajuana"amesema Dkt,Mpango
Aidha Dkt,Mpango ameagiza wizara ya Fedha kuhakikisha inatafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya kutoka kipande cha kutoka Lutukila kufika Makambako kwa kuwa chakula kingi kinatoka mikoa ya kusini.
No comments:
Post a Comment