Spika wa Bunge la Tanzania na Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Machi 14, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Duarte Pacheco, wakati alipomtembelea katika Ofisi ndogo za Rais huyo zilizopo katika Ukumbi wa Mikutano wa Exhibition World Bahrain wakati wa Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani kwa nia ya kusalimiana na kuboresha ushiriki wa Tanzania ndani ya Umoja huo.
Spika wa Bunge la Tanzania na Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiagana na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Duarte Pacheco, wakati alipomtembelea katika Ofisi ndogo za Rais huyo zilizopo katika Ukumbi wa Mikutano wa Exhibition World Bahrain wakati wa Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani kwa nia ya kusalimiana na kuboresha ushiriki wa Tanzania ndani ya Umoja huo.
No comments:
Post a Comment