HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 15, 2023

ZIARA YA CHONGOLO IMEZAA MATUNDA SIMANJIRO - ANNA SHININI

 


Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MWENYEKITI wa Jumuiya ya wanawake (UWT) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Anna Shinini amesema ziara iliyofanywa na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwenye Wilaya ya Simanjiro imezaa matunda kwa jamii ya eneo hilo.

Shinini ameyasema hayo wakati akizungumza na wanawake wadau wa madini ya Tanzanite walipomwalika kwenye maadhimisho yao yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani.

Amesema ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Chongolo imekuja na mafanikio kwa jamii kwani maendeleo yatapatikana kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo itakayofanywa na Serikali.

“Serikali inayoongozwa na CCM chini ya jemedari wetu Rais Samia Suluhu Hassan itafanikisha maendeleo hayo baada ya ziara ya Kataibu Mkuu wa CCM aliyofanya hivi karibuni,” amesema Shinini.

Amesema Chongolo amewaahidi maendeleo mbalimbali kwenye sekta ya maji, miundombinu ya barabara na afya kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Simanjiro.

“Ametuahidi ujenzi wa hospitali kwenye mji mdogo wa Mireani, barabara mbili za kutoka Mirerani hadi Orkesumet na Arusha hadi Orkesumet, kisha Kiteto hadi Kongwa, hivyo tukae mkao wa kula,” amesema Shinini.

Amesema pia suala la usambazaji wa maji kwenye mji mdogo wa Mirerani, Katibu Mkuu wa CCM Chongolo amelizungumza na kuwaeleza wananchi watafaida na huduma hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Light In Africa, Shinini amewaahidi watoto hao kuwasaidia kupitia shirika lake lisilo la kiserikali.

“Huwa natembelewa na wageni kutoka nje ya nchi na wanapenda kutoa misaada kwa watoto hivyo nawaahidi mwaka huu msaada watakaotoa tutafikisha kwa watoto wa Mirerani badala ya Arusha,” amesema.

Shinini baada ya kutembelea kituo hicho amejitolea shilingi 100,000 kwa ajili ya watoto hao na kuiasa jamii kuwajali watoto wenye kuishi katika mazingira hatarishi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad