HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 1, 2022

WADAU WAKUTANA DAR ES SALAAMA KUJADILI NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 Na.Khadija Seif,Michuzi TV 

MJADALA wa Kitaifa wa Nishati safi ya kupikia umefunguliwa rasmi leo November Mosi Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) n kwa siku 2 ikiwahusisha wadau,taasisi mbalimbali kwa lengo la kujadili matumizi ya Nishati safi ya kupikia.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo Novemba mosi Katibu Mkuu wizara ya Nishati  Felchesmi Mramba amesema tukio la mjadala huo unafanyika mikoa mbalimbali  ikiwemo Tabora,Shinyanga, Iringa,Dodoma na Morogoro huku takribani mamilioni ya watanzania wakifatilia kupitia televisheni na mitandao ya kijamii.

Aidha, Mramba ameeleza kuwa mjadala huo ni safari ya awali ya kuhama kwenye nishati isiyo salama ya kupikia na kuelekea nishati safi ya kupikia .

"Tunatambua madhara yanayopatikana kwa kutumia nishati ya kupikia isiyo salama na inaleta madhara mbalimbali ikiwemo athari kiafya,kiuchumi,kijamii hivyo wadau na taasisi zitajadili namna ya taifa litahamia kwenye nishati safi ili kuepuka matatizo yanayopatikana kwani waathirika ni vielelezo tosha kuwa changamoto bado zinaendelea na jamii bado haijapata uelewa wa namna ya kukabili changamoto za nishati isiyosalama.

Hata hivyo mjadala huo umehusisha  wadau,taasisi na viongozi mbalimbali  kiserikali  pamoja na viongozi wastaafu. 

Pia Mramba amefafanua kuwa kuwepo kwa mjadala huu wa siku 2 ni ishara ya wazi kuwa lengo la kumtua mama kuni kichwani litapata Suluhisho.

Mtaalam mwandamizi wa maswala ya Fedha katika shirika la umoja wa mataifa wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) Immanuel Muro akichangia mjadala wa kupatikana kwa Suluhisho la kitaifa la Nishati safi ya kupikia na kueleza kuwa bado asilimia kubwa jamii  haina elimu ya kuelewa madhara yanayopatikana katika nishati isiyo salama ya kupikia na kuepelekea matumizi ya mkaa na kuni kuendelea kwa baadhi ya jamii.

Hata hivyo Muro amesema kuwa ukosefu wa maji safi katika mkoa wa Dar es salaam inawezwa kusababishwa na kukatwa kwa miti na misitu kwani mikoa ya Lindi,Mtwara, Morogoro ndio mikoa inayotiririsha Maji kufika mkoa wa Dar es salaam .

"50% ya wakazi wa Dar es salaam wanatumia mkaa kam nishati ya kupikia  ambapo miaka mitano ijayo changamoto za kiafya zitazidi pamoja na changamoto ya kimazingira itakbiliwa na ukame."

Pia ametoa rai kwa Serikali kutafuta ufumbuzi  wa haraka na kuhakikisha jamii inapata uelewa na kutambua madhara yanayosababishwa na matumizi ya Nishati ya mkaa na kuni.

Kwa upande wake waziri mstaafu na Mkurugenzi mkuu mstaafu wa shirika la umoja wa mataifa wa Makazi duniani (UN_Habitat) Anna Tibaijuka amesema yeye ni mmoja ya mashuhuda wa watumiaji wa nishati ya kupikia ya kuni na kukiri kuwa ametembea porini kutafuta kuni.

"Tuzungumze mkakati wa kitaifa wa kuondokana na kuweza kupikia Nishati safi kiwe kikao cha mkakati. Mpangilio ni nzuri na wale walio kwenye TV wanaona kwamba Serikali yetu ina mpango Kwa kutusaidia akina mama."

Aidha,Tibaijuka ametoa rai kwa  serikali kuweka mkakati wa sera ya kitaifa ya kuweka bei isiyobadilika badilka,mpango huu using kuwa kama Agizo tu Bali liwe na mpango, sera na mazingira wezeshi kwa watu kumudu gharama hizo.

Katibu Mkuu wizara ya Nishati  Felchesmi Mramba, Akizungumza juu ya Umuhimu wa Mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi.

Mtaalam mwandamizi wa maswala ya Fedha katika shirika la umoja wa mataifa wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) Immanuel Muro Akizungumza juu ya umuhimu wa Nishati Safi na namna Mkaa unavyochangia  kuharibu Mazingira
Mkurugenzi wa Taifa Gesi, Hamisi Ramadhani akichnagia katika Mjadala wa  Kitaifa waNishati Safi ya Kupikia .uliofungiliwa leo jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Nishati ,January Makamba akiongoza Mjadala wa Kitaifa juu ya Masuala ya Nishati Safi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Waziri na Mbunge Mstaafu ,Prof .Anna Tibaijuka akichangia mada ni namna gani jamii inaweza kubadilika na kuanza kutumia Nishati Safi .




1 comment:

  1. Sisi Ishai Real Estate na Ishai Company Ltd tumeshiriki pamoja na Mkurugenzi wetu Mr Johnson Yesaya Mgelwa katika uzinduzi wa mjadala wa kitaifa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia leo 01/11/2022.

    Tunaunga mkono wazo la serikali kuja na mpango wa kuachana na matumizi ya mkaa pamoja na kuni na kuhamia katika matumizi ya nishati zingine kama gesi, umeme, jua na bio-gas kwa lengo la kulinda afya ya mwanamke ambaye ndiye muathirika mkuu wa athari za kiafya zitokanazo na kuni na mkaa.

    Tutashiriki kikamilifu katika agenda hii. http://www.ishai.co.tz

    ReplyDelete

Post Bottom Ad