TRA Washauriwa kutumia Mbinu mbadala ya kuwadhibiti wafanyabiashara wadanganyifu - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 1, 2022

TRA Washauriwa kutumia Mbinu mbadala ya kuwadhibiti wafanyabiashara wadanganyifu

Afisa mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA), Adeotus Kabuteni akitoa elimu ya mlango kwa mlango katika kampeni inayoendelea katika mkoa wa Simiyu kwa lengo kuelimisha wafanyabiashara wa mkoa huo sambamba na kuskiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Bw. Gabriel Zakaria, akizungumza na maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzan(TRA) walipomtembelea kwaajili ya kupata utambulisho rasmi ili waweze kutoa elimu ya mlango kwa mlango katika kampeni inayoendelea katika mkoa wa Simiyu kwa lengo kuelimisha wafanyabiashara wa mkoa huo sambamba na kuskiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.
Afisa Mkuu wa Kodi TRA, Peter Shewio akizungumza na mfanyabiashara  wakati akitoa elimu ya mlango kwa mlango katika kampeni inayoendelea katika mkoa wa Simiyu kwa lengo kuelimisha wafanyabiashara wa mkoa huo sambamba na kuskiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Maafisa kutoka TRA wakiotoa elimu kwa wafanyabiashara wa lamadi wilaya ya Busega Mkoani Simiyu
Afisa msaidizi wa Kodi TRA, Chama Siriwa elimu ya mlango kwa mlango katika kampeni inayoendelea katika mkoa wa Simiyu kwa lengo kuelimisha wafanyabiashara wa mkoa huo sambamba na kuskiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

MKUU wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Bw. Gabriel Zakaria ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutumia Mbinu mbadala ya kuwadhibiti wafanyabiashara wadanganyifu, wanaowashawishi wanunuzi kutokudai risiti kwa madai ya kuwapunguzia bei ya bidhaa wanazonunua na kutoa risiti zenye thamani pungufu.

Ameyasema hayo alipotembelewa na ugeni wa Maafisa wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) uliongozwa na Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi, Bw. Julius Mjenga kwa lengo la kujitambulisha kwa Mkuu huyo kabla ya kuanza kwa zoezi la elimu ya mlango kwa mlango katika kampeni inayoendelea katika mkoa wa Simiyu kwa lengo kuelimisha wafanyabiashara wa mkoa huo sambamba na kuskiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Bw. Zakariya alianisha kuwa katika siku za karibuni kumekuwa na mbinu kadhaa zinazotumiwa na wafanyabiashara katika utoaji wa risiti halali jambo ambalo linasababisha upotevu wa mapato ya serekali.

Mingoni mwa Mbinu hizo ni kutotoa risiti kwa wateja kwa madai ya kuwapunguzia bei ya bidhaa wanazonunua, kuwapa wateja wao risiti pungufu zisizolingana na bei halisi ya bidhaa hizo na kuwatafutia risiti nyengine kabisa zinazonesha bidhaa nyengine tofauti kabisa na wateja wanazonunua.

Aidha, Mkuu huyo ametoa rai ya kutumia mbinu za kuiwandishi wa habari za uchunguzi kuwabaini wote wanaofanya mitindo hiyo kwa kuwaweka wazi kwenye vyombo vya habari na kuwachukulia hatua za kisheria ili iwe funzo kwa wengine kwa kufanya hivyo kutapunguza udanganyifu huo na kuwezesha TRA kufikia au kuvuka kabisa ya malengo ya makusanyo.

Pia, Bw. Zakariya amewapongeza TRA kwa makusanyo makubwa na jitahada zao na kuendelea kutoa elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara pamoja na kusikiliza changamoto zao na kuwataka waendelee na jitihada hizo jambo ambalo litaongeza ulipaji wa Kodi kwa hiari na kuchochea zaidi kasi ya ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Kwa upande wake Bw. Julius Mjenga amesema kuwa zeozi linaendelea vizuri mkoani humo na wamekua wakipokea changamoto na maoni kadhaa kutoka kwa wakuu wa mikoa na wafanyabiashara mkani humo ikiwemo kusongezewa huduma katika maeneo yao ili kurahisisha ulipaji wa kodi kwa hiari na kuwapunguzia gharama za usafiri.

Timu ya maafisa ya TRA inaendelea na Kampeni yake ya Elimu ya mlango kwa mlango ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuhitimishwa mishoni mwa wiki wilayani Miatu mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad