HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 19, 2022

Mshindi wa jackpot ya katikati ya wiki wa 10bet apatikana

 
Na Mwandisho wetu


Dar es Salaam. Shabiki wa klabu ya Simba na Liverpool ya England Richard Mkumbo ameshinda Sh11 milioni kupitia jackpot ya katikati ya wiki ya kampuni ya 10bet Tanzania.

Mkumbo ambaye ni mkazi wa Singida ameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 10 za ligi mbalimbali duniani kwa sh500 tu.

ameshametia kibindoni Sh11 milioni kati ya jackpot ya 10bet Tanzania katikati ya wiki, na kumfanya kuwa mshindi wa kwanza kuwahi kutokea Tanzania.

Mkumbo alitia kibindoni kiasi hicho baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 10 za ligi mbalimbali duniani akiwa na Sh500 pekee.

Ushindi huo unamfanya Mkumbo kuwa mshindi wa kwanza wa jackpot hiyo hapa nchini na kukakabidhiwa zawadi yake na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, George Abdulrahman katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jana.

Mkumbo alisema aliamua kubashiri na 10bet kwa sababu kuwa na ‘odds’ iliyowekwa na kampuni hiyo katika mechi mbalimbali.

“Mimi ni mjasiriamali na nimekuwa nikibashiri na 10bet mara kadhaa na sikushinda. Hata hivyo sikukata tamaa na kuendelea na kufanikiwa kushinda milioni 11 kwa sh500 tu,” alisema Mkumbo.

Mshindi huyo aliwaomba vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na kampuni hiyo ili kushinda fedha kwa dau dogo tu.

"Ndoto yangu imetimia kwa sababu lengo la kubashiri na 10bet ni kushinda na nimefanikiwa, nitaendelea kubashiri na kampuni hii," alisema.

Alisema atazitumia fedha hizo kuendeleza biashara zake Dar es Salaam na Singida huku akisaidiana ndugu zake katika masuala ya elimu.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa 10bet Tanzania George Abdulrahman alisema wanajisikia fahari sana kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo yao ya kubashiri.

Kwa mujibu wa Abdurahman, Watanzania wengi wamekuwa wakitabiri na kujishindia fedha kupitia michezo yao ya kubashiri na kufanya mambo ya maendeleo.

Meneja Masoko wa kampuni ya 10bet Tanzania George Abdulrahman (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 11 kwa Richard Mkumbo ambaye amekuwa mshindi wa kwanza wa jackpot ya katikati ya wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad