HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 19, 2022

Mkazi Songea ajishindia bodaboda kupitia NMB MastaBata Kotekote, Wengine 75 wazoa zaidi ya Milioni 7

 

Benki ya NMB imepata mshindi wa pili wa bodaboda, Charles Erasto Mbwilo kutoka Songea Mkoani Ruvuma kupitia droo ya shindano la NMB MastaBata Kote-kote.

Katika kampeni hiyo ambayo jumla ya Sh350 Milioni zitatolewa kwa washindi 854 ikiwa ni pamoja na Zawadi za Pikipiki na safari ya Dubai kwa washindi saba pamoja na wenza wao.

Akizindua droo ya pili ya mchezo huo katika Tawi la NMB - Mkwawa, Mkoani Iringa, Kaimu Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Manyilizu Masanja alisema lengo kubwa ni kuhamasisha matumizi ya NMB mastercard na Lipa Mkononi(mastercard QR) kwa wateja wake.

Masanja alisema wateja wakifanya miamala yao kupitia kadi ya NMB mastercard au Lipa Mkononi(mastercard QR) au mtandaoni watakuwa wamejiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya ushindi katika droo zijazo.

Naye, Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi, Manfred Kayala aliwahimiza wateja kuendelea kutumia njia hiyo kufanya miamala ili waingie kwenye droo hiyo na baadae kushinda.

Kwa upande wake mshindi wa bodaboda wa wiki iliyopita, Asumwisye Mwajeka baada ya kukabidhiwa zawadi yake akisema;

"Niwahamasishe vijana wenzangu msitembee na pesa mikononi au mifukoni, faida yake mimi nimeiona. Nimefurahi kupata bodaboda," alisema.

Tayari Sh15 Milioni zimetolewa kwa washindi 150 mpaka sasa na bodaboda mbili zikiwa na thamani ya Sh6 Milioni.

Mshindi wa kwanza wa Bodaboda katika Kampeni ya Mastabata – Kotekote ya Benki ya NMB, Asumwisye Mwajeka (wapili Kushoto) akiijaribu pikipiki baada ya kukabidhiwa katika benki ya NMB tawi la Mkwawa Mkoani Iringa. Kushoto ni Meneja mwandamizi wa Idara ya Biashara za Kadi, Manfredy Kayala, kulia ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mkwawa, Happiness Pimma na wapili kulia ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu, Manyilizu Masanja



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad