HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 19, 2022

TPDC YALAZIMISHWA SARE NA BMH MICHUANO YA SHIMUTA TANGA

Kikosi cha timu ya TPDC kilichocheza dhidi ya BMH leo kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Tanga School. KOCHA wa timu ya TPDC Bizoo Bituka akitia maelekezo kwa wachezaji wake


Na Oscar Assenga,TANGA.
TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imelazimishwa sare tasa ya kutokufungana na timu ya Benjamini Mkapa Hospitali (BMH) ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi Jijini tanga.

Mchezo huo uliochezwa kwenye Dimba la Shule ya Sekondari Tanga Ufundi ulikuwa wa aina yake kutokana na kila timu kutaka kuondoka na alama tatu na hivyo kuzidisha upinzani .

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Kocha wa timu ya TPDC Bizoo Bituka amesema malengo yake makubwa ilikuwa ni kupata pointi tatu muhimu lakini hata pointi moja aliyoipata wanashukuru.

Alisema pamoja na uwepo wa ushindani katika michuano hiyo lakini wao wamejipanga na kujiimarisha kuhakikisha wanapata alama tatu kila mchezo ili kuweza kutimiza malengo yao ya kunyakua ubingwa wa mchezo huo.

Sehemu ya kikosi ambacho kiliwakilisha timu ya TPDC katika mchezo wa leo ni Nahodha Dalushi Shija, Oscar Mwakasege, Peter Ngalu, Mwikabe Muhono.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad