HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 30, 2021

Uwekezaji katika Tafiti za Kisayansi kuchangia kufikia Maendeleo Endelevu

 

Na Mwandishi wetu, Morogoro

WAKATI Tanzania imeamua kuwa nchi ya viwanda kumeelezwa uwapo wa haja  ya kufanyika kwa marekebisho ya kutosha katika sera ya elimu  na uwapo  wa sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuongeza kasi ya ubunifu nchini unaozingatia uwezo wa kisayansi aliokuwa nao mhusika na nafasi wazi za ushindani zinazosaidiwa na sera.

Kauli hiyo ilitolewa na baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo juu ya program ya GO-SPIN ambayo inatumika kama miongoni mwa zana muhimu za UNESCO za kujengea nchi wanachama uwezo wa kuchambua sera ili kugundua mapungufu na kuanzisha mageuzi na uboreshaji wa mifumo na utawala wake. Warsha hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA).

Wakizungumza katika warsha hiyo iliyoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Visiwani Zanzibar, wamesema kwamba kukosekana kwa sera sahihi ya elimu na ya sayansi na ubunifu kumefanya ushawishi wa ushiriki katika sayansi na ubunifu kuwa mdogo.

Ofisa Mhakiki Ubora Mkuu wa TCU, Dk Fulgence Matimbo alisema kwamba kuna haja kubwa ya kufanya marekebisho ya sera na sheria zilizopo ili kuwezesha vijana kuingia katika kasi ya ubunifu na sayansi kupitia mpango wa utoaji wa elimu mtandaoni ambao utatambulika kisheria na kisera.

Alisema katika utafiti walioufanya waliandika mapendekezo ya marekebisho kadhaa katika mitaala na sera lakini walielezwa wazi kuwa wao kwa mujibu wa sheria iliyoanzishwa hawahusiki na hivyo kupeleka mapendekezo yao kwa wahusika ambao hayajafanyiwa kazi hadi leo.

“Elimu yetu ya sasa inahitaji uso kwa uso yaani uone madarasa, uone madawati na kubwa zaidi uone uwapo wa mtu darasani. Dunia kwa sasa haipo hivyo. Tulimleta mtaalamu kutusaidia lakini alipouliza online delivery programme sisi tukawa tunazungumzia face to face” alisema Dk Matimbo na kuongeza kuwa kutokuwepo kwa hali hiyo kunawafunga vijana wengi katika madarasa na wale ambao ni welevu wa haraka kuchelewa kukua.

Alisema ipo haja elimu kuwa na mnyumbuko wa kutambua wanaojifunza kwa kasi na kuwafanya waweze kukamilisha kasi yao kwa muda muafaka.

“tumetengeneza waraka kuhusu hili la mabadiliko lakini wenzetu wakenya wakaja kuchukua na kulifanyia kazi sisi tulikopeleka ushauri mpaka leo  hakuna kilichofanyika na wenzetu wanakimbia katika utoaji wa elimu kwa watu wao na kuwekeza katika ubunifu” alisema Dk Matimbo.

Alisema Watanzania wapo wazuri katika kufanya utafiti na kuibua mambo yanayostahili kufanyika kuleta mabadilio chanya lakini si watekelezaji wa tafiti hizo, alisema Dk Matimbo.

Kauli hiyo iliungwa mkono na muaandishi wa habari muaandamizi, Thom Chilala ambaye alisema tafiti nyingi haziwafikii wahusika kutokana na watafiti kufungia kazi zao makabatini na kuwataka kuziweka wawazi ili waandishi waweze kuwapatia wananchi.

Alisema kufichwa kwa tafiti hizo kunazuia  kufikiwa kwa malengo na pia kutambuliwa kwa wanasayansi  ikiwa ni pamoja na wale wa sayansi asili ambayo ni muhimu kwa suala la ubunifu.

Naye Mbunge wa viti maalumu Mh. Nusrat Hanje ambaye ni miongoni mwa wabunge walioshiriki warsha hiyo alisema mradi wa UNESCO umekuja wakati sahihi kwani sera ya sayansi inayoitumika sasa ipo nyuma miaka 25 na inazuia maendeleo katika eneo hilo.

Alisema kuna haja ya kubadili mfumo wa elimu ili ujenge uwezo wa sayansi na ubunifu ili teknolojia iweze kutumika kuboresha maisha ya wananchi.

Aliitaka serikali kuweka nguvu katika kuhakikisha vijana wanakua na tafakari tunduizi ili kuonesha njia ya ustawi katika sayansi.

“sasa hivi tunarekebisha sera ya sayansi na mtaala kwa pamoja. Hatupaswi kufanya hivyo tunatakiwa kutengeneza sera kwanza kisha tuwe na mtaala ili tujue katika miaka 20 ijayo tunataka nini” alisema Nusrat.

Naye Omary Salehe kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar alisema ukiangalia mwenendo wa taifa utabaini kwamba kuna kasoro kubwa katika kuimarisha ubunifu hasa pale wabunifu wanapokosa kuendelezwa kutokana na kukosekana kwa sera na nini kifanyike kwa wagunduzi na wanasayansi.

Anasema kuna shida kubwa kwa wabunifu kutopata msaada, lakini anaona kwamba yote yanasababishwa na kukosekana kwa sera madhubuti na utashi wa kusaidia wagunduzi.

Alitolea mfano wa mgunduzi mmoja Zanzibar ambaye alianza katika gari, kisha baluni na baadaye helkopta iliyosafiri mpaka Dar es salaam katika miaka ya 2017 na 2018 lakini mpaka leo hajulikani alipo wala mwendelezo wa ubunifu wake.

“Ni lazima tutengeneze utaratibu kupitia sera, tusaidie wagunduzi hawa na tuupeleke ugunduzi wao mbali zaidi ili kila mtu aone faida ya kufikiri kichanya katika sayansi teknolojia na ubunifu” alisema Salehe.

Alisema kugundua na kuuza ni vitu viwili tofauti lakini kama taasisi na wadau wengine wote watashirikishwa katika sera na kujua njia sahihi taifa hili litajivunia nguvu kazi yenye kufikiri mbali zaidi ya hapa tulipo.

Awali mratibu wa mradi huo ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia kutoka UNESCO, Bw. Keven Robert alisema kuwa mradi huo utasaidia wananchi kuwa na hamu ya sayansi na hivyo kusaidia nchi kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na utafiti.

Aidha mradi huo pia utasaidia kuimarisha taasisi za kisayansi kufanya tafiti na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti za kisayansi ambazo zitasaidia katika kutatua changamoto za wananchi, kukabiliana na majanga yakiwemo magonjwa mbalimbali na pia kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Robert alisema kuwa mradi huo utakuwa na maeneo 10 ya utekelezaji ambapo baadhi ya maeneo ni pamoja na kuangalia uwekezaji katika tafiti za kisayansi ambapo matokeo ya tafiti hizo zinapouzwa zinaweza kuimarisha uchumi ya nchi.

“Mfano katika kipindi hiki cha janga la Corona yapo mataifa yaliyofanya tafiti za kisayansi na kutengeneza chanjo hivyo zinapouzwa mataifa hayo yamekuwa yakipata fedha na kukua kiuchumi,” alisema Robert.

Alitaja maeneo mengine yatakayoangaliwa katika mradi huo kuwa ni kwa namna gani tafiti za kisanyansi zinasaidia wananchi na kwa namna gani wananchi wanashirikishwa kwenye tafiti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Mkuu wa Kitengo cha Sayansi Asili –UNESCO na Mratibu wa Mradi Unaofadhiliwa na SIDA akitoa mada wakati wa Mafunzo ya Kuimarisha Mifumo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Mratibu wa Mradi wa kuboresha mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA), Bw. Keven Robert akiwasilisha mada inayoelezea mradi huo wakati wa warsha ya mafunzo juu ya program ya GO-SPIN ambayo inatumika kama miongoni mwa zana muhimu ya UNESCO ya kujengea nchi wanachama uwezo wa kuchambua sera ili kugundua mapungufu na kuanzisha mageuzi na uboreshaji wa mifumo na utawala wake inayoendelea mjini Morogoro.
Mbunge wa jimbo la Kwahani kutoka Zanzibar Mh. Yahya Rashid Abdulla akishiriki wakati wa warsha ya mafunzo juu ya zana ya UNESCO chombo cha uchunguzi wa kimataifa juu ya sera ya sayansi na vyombo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa ufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) inayoendelea mjini Morogoro.
Mbunge wa viti maalumu (Chadema) Mh. Nusrat Hanje akichangia mada wakati wa warsha ya mafunzo juu ya program ya GO-SPIN ambayo inatumika kama miongoni mwa zana muhimu ya UNESCO ya kujengea nchi wanachama uwezo wa kuchambua sera ili kugundua mapungufu na kuanzisha mageuzi na uboreshaji wa mifumo na utawala wake iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa ufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) inayoendelea mjini Morogoro.
Ofisa Mhakiki Ubora Mkuu wa TCU, Dk Fulgence Matimbo akichangia mada wakati wa warsha ya mafunzo juu ya program ya GO-SPIN ambayo inatumika kama miongoni mwa zana muhimu ya UNESCO ya kujengea nchi wanachama uwezo wa kuchambua sera ili kugundua mapungufu na kuanzisha mageuzi na uboreshaji wa mifumo na utawala wake iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa ufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) inayoendelea mjini Morogoro.
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel akizungumza wakati wa warsha ya mafunzo juu ya program ya GO-SPIN ambayo inatumika kama miongoni mwa zana muhimu ya UNESCO ya kujengea nchi wanachama uwezo wa kuchambua sera ili kugundua mapungufu na kuanzisha mageuzi na uboreshaji wa mifumo na utawala wake iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa ufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) inayoendelea mjini Morogoro.
Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Mratibu wa Mradi wa kuboresha mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA), Bw. Keven Robert akiwasilisha maazimio kumi kuhusu sayansi na utafiti ya mwaka 2017 wakati wa warsha hiyo inayoendelea mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo juu ya program ya GO-SPIN ambayo inatumika kama miongoni mwa zana muhimu ya UNESCO ya kujengea nchi wanachama uwezo wa kuchambua sera ili kugundua mapungufu na kuanzisha mageuzi na uboreshaji wa mifumo na utawala wake iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa ufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) inayoendelea mjini Morogoro.
Picha ya Pamoja 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad