WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUIPATIA VITENDEA KAZI (COMPUTERS) TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI CMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 30, 2021

WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUIPATIA VITENDEA KAZI (COMPUTERS) TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI CMA

 

NA KHALFAN SAID, K-VIS BLOG, MBEYA

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kuipatia vitendea kazi (computers) Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili kuharakisha shughuli za usuluhishi wa migogoro ya kikazi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mhe. Waziri wakati akikabidhi computer 10 kwa Mkurugenzi Mkuu  wa CMA, Bw.Shanes Nungu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Mbeya Novemba 29, 2021.

“Tunashuhudia hapa Workers Compensation Fund (Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi) unafanya kazi nzuri ya kuiwezesha CMA ili itekeleze majukumu yake sawasawa jambo hili lina tija katika utendaji.” Alifafanua Mhe. Waziri.

Kipekee napenda kuwashukuru sana sana wakuu wote na viongozi wa taasisi zote Dkt. John Mduma Mkurugenzi Mkuu wa WCF na ndugu Shanes Nungu Mkurugenzi Mkuu wa CMA kwa kuona umuhimu wa kufanya kazi kama serikali moja, ninyi wote mko chini ya umbrella (mwamvuli) mmoja, hakikisheni kwamba mmoja anapogundua changamoto ya mwenzake anaamua kusimama pamoja naye na kumsaidia, Alisisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama

Mhe. Waziri Jenista alisema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa ukifanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake tangu uanzishwe miaka sita iliyopita. "Kwa sheria iliyokuwepo kabla ya kupata uhuru, ilikuwa mfanyakazi akiumia analipwa fidia ya shilingi 108,000/= bila kujali amepata ulemavu wa aina gani, kwani malipo ya fidia yalikuwa kwenye flat rate". Alieleza.

Serikali iliamua kuboresha fidia kwa Wafanyakazi kwa kuanzisha mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) amba umechukua jukumu la kulipa fidia stahiki kwa mfanyakazi atakayepatwa na madhara wakati kutokana na kazi. Alibainisha

Alisema katika muktadha huo huo wa kugawa majukumu kiutendaji  Serikali ilianzisha CMA ili ishughulike na masuala ya usuluhishi na uamuzi inapotokea migogoro kazini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma alisema, makabidhiano hayo ya ni utekelezaji wa maagizo kwani ambapo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano ndipo tunaweza kufikia malengo yetu kama Taasisi lakini pia kwa pamoja chini Ofisi moja.

“Kwa kufanya kazi kwa pamoja ndipo tunaweza kufikia malengo yetu kama taasisi lakini kwa pamoja kama ofisi yako Mheshimiwa Waziri, tunatambua kwamba mmoja wetu kama atakimbia mbio na uwezo wake alionao na akawaacha ndugu zake nyuma “hatatoboa yeye peke yake”. Alisema Dkt. Mduma.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw. Shanes Nungu alimshukuru Waziri Jenista kwa maono yake na kuwezesha CMA kupata msada huo wa computer ambapo hii ni mara ya pili kupata msada kutoka WCF.

“Mheshimiwa Waziri  maagizo yako yamemezaa matunda na sasa msada huu utakwenda kuongeza nguvu kwenye ule wa awali tulioupata mwanzo kutoka WCF ambao ulisaidia kutatua malalamiko ya wananchi na ucheleweshaji wa hukumu zao umepungua.” Alishukuru Bw. Nungu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge) Bw. Kaspar Muya, wakurugenzi wa WCF na CMA pamoja na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni NSSF, PSSSF, OSHA na Idara ya Kazi.

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (wapili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Bw. Shanes Nungu (wapili kushoto) moja kati ya computer 10 zilizotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Novemba 29, 2021 jijini Mbeya. Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Kaspar Muya (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea computer kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma ambazo zilitolewa na Mfuko kuisapoti CMA.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza kwenye hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Kaspar Muya, akimkaribisha Mhe. Waziri.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akitoa neno la utangulizi
Mkurugenzi Mkuu  wa CMA, Bw.Shanes Nungu, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano ya Umma, WCF, Bi. Laura Kunenge, wakati wa hafla hiyo.
Mfawidhi wa CMA jijini Mbeya, Bw. Mwangata Makawa akitoa neno la shukrani
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa CMA
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Kazi, Mbeya
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa OSHA
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSSSF
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF

Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad