M-Bet yamwaga Sh961m kwa washindi, Shabiki wa Yanga ashinda Sh104.3m - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 7, 2021

M-Bet yamwaga Sh961m kwa washindi, Shabiki wa Yanga ashinda Sh104.3m

 Kampuni ya mchezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imetumia jumla ya Sh milioni 961 kuzawadia washindi mbalimbali wanaobashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 na Jackpot Bonus .

Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi wakati wa kumzawadia zawadi yake Stephano Ndunguru kutoka mkoani Njombe aliyeshinda Sh104.3 millioni.

Mushi alisema kuwa Ndunduru anakuwa mshindi wa 10 kuzawadiwa mamilioni ya fedha kwa mwaka huu na kuifanya kampuni yao kutumia kiasi hicho cha fedha.

 Alisema kuwa wanajisikia faraja sana kuendelea kubadili na kuwawezesha wanamichezo kupitia michezo yao ya kubashiri na sasa kuwa na maisha bora.

“Mbali ya kubadili maisha ya washindi wetu kupitia kubashiri michezo, pia tunajisikia fahari kuchangia  asilimia 20 ya kodi ya ushindi ambayo inaigia moja kwa moja serikalini . Sisi ni walipa kodi wazuri wa serikali na tunachangia maendeleo,” alisema Mushi.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo, Sh791millioni ni zawadi za moja kwa moja kwa washindi wakati Sh200 millioni ni zawadi kwa ya ‘jackpot’ bonus. Alisema kuwa wanatarajia kuwazadia washindi wengi  mwaka huu kwani ligi mbalimbali zinaendelea mpaka sasa.

Kwa upande wake, Ndunduru ambaye ni shabiki wa Yanga alisema kuwa hakuamini kushinda kiasi hicho cha fedha kwa kutumia Sh1,000 tu. “Mimi mkulima wa maharage, nimekuwa nikibashiriki na kupata hela ndogo ndogo. Nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa nimeshinda zaidi ya milioni 100, sikuamini  na nilidhani ni ndoto,” alisema Ndunduru.

Alisema kuwa fedha hizo atazitumia kuendesha kilimo cha kisasa zaidi na kutoa ajira kwa watu wengine.

Msanii maarufu nchini Hamadi Ali 'Madee' (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 104.3  Stephano Ndundulu baada ya kubashiriki kiusahihi mechi 12 za mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad