
Wiki hiyo vile vile itajumuisha shughuli mbalimbali jijini Dar es salaam ambapo viongozi wakuu wa Tigo watatoa huduma katika kitengo cha huduma kwa wateja cha miito ya simu (Call Center) kwa masaa machache ambapo watashughulikia matatizo ya wateja.

Akiongea leo katika duka la Tigo Dodoma, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja, Mwangaza Matotola alisema kwamba wiki itakuwa na maonesho ya Huduma bora za Tigo kwa wateja wake na watoa huduma wa huduma kwa wateja.
"Mwaka huu tumekusudia kubainisha ukaribu mashuhuri wa kampuni ya Tigo Tanzania kwa wateja wake, na msisitizo wetu katika huduma kwa wateja katika wiki hii ni kwa lengo la kutambua kwamba mawakala wetu wa huduma kwa wateja ni taswira ya biashara yetu. Kutokea pale ambapo tatizo la mteja lilipo pokelewa, mpaka litakapo kuwa limetatuliwa, watoa huduma wetu wa huduma kwa wateja wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba mahitaji ya kila mmoja yamefikiwa kwa wema na furaha.

Wateja wa Tigo wanahamasishwa kutembelea maduka ya Tigo na kutumia mifumo mingine ya kidigitali; kituo cha miito ya simu (call center), WhatsApp, Instagram, Twitter na Facebook wanapokuwa wanahitaji msaada. Watahudumiwa na timu ya wataalamu wenye mafunzo.

"Kuwaridhisha wateja na kupata mrejesho ni msingi wa utendaji wetu. Tunaamini kwamba siku tutakapoacha kufanya tathmini ya biashara yetu na jinsi ambavyo huduma zetu zinavyoathiri wateja ni siku ambayo tutakosa maana ya uwepo wetu. Hii ndio sababu kwanini tunaendelea kujitolea wenyewe kuhudumia wateja wetu na kuongeza uendeshaji" alihitimisha Matotola.

No comments:
Post a Comment