HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 7, 2021

Kampuni ya Tigo Tanzania Yadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2021

Tarehe 4 Oktoba 2021. Kampuni ya kidigitali inayoongoza Tanzania, Tigo iliadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu kwa shamra shamra za kipekee.  Wiki ya huduma kwa wateja ilianza kwa matembezi mafupi katika mitaa ya mji wa Dodoma, kisha baadae kuelekea katika uzinduzi rasmi wa wiki ya CSW, ambayo ilihitimishwa na chakula cha machana pamoja na wateja waaminifu.  
 
Wiki hiyo vile vile itajumuisha shughuli mbalimbali jijini Dar es salaam ambapo viongozi wakuu wa Tigo watatoa huduma katika kitengo cha huduma kwa wateja cha miito ya simu (Call Center) kwa masaa machache ambapo watashughulikia matatizo ya wateja. 
Sherehe za wiki nzima zitaenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu:  "Power of Service" ambayo inabainisha jinsi timu ya huduma kwa wateja ilivyoweza kukabiliana na mazingira ya kutoka kufanya kazi ofisini kwenda kufanya kazi nje ya ofisi katika kipindi cha janga la ugonjwa wa uviko.  
Akiongea leo katika duka la Tigo Dodoma, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja, Mwangaza Matotola alisema kwamba wiki itakuwa na maonesho ya Huduma bora za Tigo kwa wateja wake na watoa huduma wa huduma kwa wateja.   

"Mwaka huu tumekusudia kubainisha ukaribu mashuhuri wa kampuni ya Tigo Tanzania kwa wateja wake, na msisitizo wetu katika huduma kwa wateja katika wiki hii ni kwa lengo la kutambua kwamba mawakala wetu wa huduma kwa wateja ni taswira ya biashara yetu.  Kutokea pale ambapo tatizo la mteja lilipo pokelewa, mpaka litakapo kuwa limetatuliwa, watoa huduma wetu wa huduma kwa wateja wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba mahitaji ya kila mmoja yamefikiwa kwa wema na furaha. 
"Kama ilivyo kwa kauli mbiu ya mwaka huu, Katika kampuni ya Tigo tunatilia mkazo katika nguvu ya huduma, jinsi ambavyo tunabadilika kuendana na mabadiliko yatokanayo na Uviko 19, na hii ndio sababu kwanini tunasisitiza katika kutoa huduma za kuaminika na zenye ufanisi kwa wateja wetu kila siku, jambo hili lilidhihirishwa na timu yetu ya huduma kwa wateja katika mikoa mbalimbali nchini". alisema Matotola. 

Wateja wa Tigo wanahamasishwa kutembelea maduka ya Tigo na kutumia mifumo mingine ya kidigitali; kituo cha miito ya simu (call center), WhatsApp, Instagram, Twitter na Facebook wanapokuwa wanahitaji msaada.  Watahudumiwa na timu ya wataalamu wenye mafunzo.
Sherehe hizo ambazo zitadumu kwa wiki nzima ni matokeo ya jitihada za kampuni ya Tigo kuongeza ushirikiano na wafanyakazi.  Zaidi ya ushiriki wa timu ya viongozi wa juu, watoa huduma kwa wateja wote katika maduka ya Tigo na vituo vya call center watapata keki ya pongezi na zawadi zingine kwa kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza kutoa huduma na utayari wa kuleta wema na furaha kwa wateja wote wa Tigo nchini. 

"Kuwaridhisha wateja na kupata mrejesho ni msingi wa utendaji wetu.  Tunaamini kwamba siku tutakapoacha kufanya tathmini ya biashara yetu na jinsi ambavyo huduma zetu zinavyoathiri wateja ni siku ambayo tutakosa maana ya uwepo wetu.  Hii ndio sababu kwanini tunaendelea kujitolea wenyewe kuhudumia wateja wetu na kuongeza uendeshaji" alihitimisha Matotola.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad