ZABUNI 39,716 ZENYE THAMANI YA Tsh.TRILIONI 24.07 ZIMEOROTHESHWA PPRA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 3, 2021

ZABUNI 39,716 ZENYE THAMANI YA Tsh.TRILIONI 24.07 ZIMEOROTHESHWA PPRA

 

Mkurugenzi wa PPRA Mhandisi Leonard Kapongo akizungumza katika mkutano wa nane wa usimamizi wa ununuzi wa umma uliofanyika Jijini Arusha katika kituo Cha kimataifa Cha mikutano AICC
Mgeni rasmi katika mkutano wa nane wa usimamizi wa ununuzi wa umma Dkt Khatib kazungu Naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipangoNa.Vero Ignatus Arusha


Mkutano wa nane wa usimamizi wa ununuzi wa umma umefanyika Jijini Arusha, ukiwa na lengo la washiriki kupata Elimu juu ya masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nyenzo na miongozo ya ununuzi wa umma iliyotolewa na Serikali ambayo hutumika katika michakato ya ununuzi.

Mhandisi Leonarld S.Kapongo ni Mkurugenzi wa PPRA, anasema kuwa kongamano hilo linafanyika baada ya kutoa mafunzo ya Sheria ya ununuzi wa umma kwa watendaji takribani 2,300,kutoka katika Taasisi nunuzi 310,mafunzo kwa mfumo wa ununuzi kwa niia ya mtandao kwa washiriki 239 ikijumuisha mafunzo maalum kwa Taasisi nunuzi na mafunzo ya pamoja ya mfumo

Jumla ya taasisi nunuzi 557 sawa na asilimia 98 ya taasisi zote za ununuzi zimekwisha unganishwa katika mfumo wa TANePS na Jumla ya wazabuni 19,557wamekwishasajili katika mfumo huo, ambapo kufikia robo tatu ya mwaka wa fedha Jumla ya zabuni 39,716 zenye thamani ya Tsh.Trilioni 24.07zikiwa zimeorotheshwa.

Alisema PPRA unaendelea kuweka juhudi katika kuhakikisha kuwa Taasisi zote nunuzi zinaungamishwa kwenye mfumo,ikiwa ni pamoja na asilimia 2.3 ya taasisi ambazo hazijaunganishwa kwenye mfumo .

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika mkutano wa nane wa usimamizi wa ununuzi wa umma Dkt Khatib kazungu Naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango aliwataka washiriki kuelewa kuwa wanahusika kwa namna mbalimbali kutekeleza shughuli za ununuzi kwenye taasisi zao kwa kuzingatia Sheria , kanuni na taratibu za ununuzi wa umma

Amewataka kutambua kuwa wanao wajibu wa pamoja ,kila mmoja kwanafasi yake kuhakikisha kuwa mchakato inayoitia katika mikono yao inafanywa kwa uzalendo ,uadilifu na kwa ufanisi mkubwa ili fedha zinazotumika ziweze kuleta manufaa kwa walengwa ambao Ni wananchi .

Nae Mjimbe wa bodi mwakilishi wa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya PPRA Prof.Sufian Bukurura alisema kuwa kongamano Hilo lengo kuu Ni kuwakutanisha wadau,kubadilishana uzoefu kujifunza kujadili Mambo muhimu yahusuyo sekta ya ununuzi wa umma kwa ujumla kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta hiyo muhimu kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania

Aliweza kuorothesha changamoto mbalimbali zinazoikabili PPRA ikiwa Ni pamoja na baadhi ya taasisi za umma kutokutoa ushirikianowakati wa ukaguzi,baadhi ya taasisi kutowasilisha ripoti kwanwakati,baadhi ya taasisi za Serikali kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mikataba ya ununuzi na kukwamisha thamani halisi ya fedha,kukosekana kwa msawazisho wa bidhaa na huduma zinazotumika serikalini

Kongamano hilo limekuwa likifanyika kila mwaka kwa miaka Saba mfululizo yaani kuanzia mwaka 2013 hadi 2019,Hata hivyo kwa mwaka huu wa fedha 2019-2020 kongamano Hilo halikufanyika chini ya Wizara ya fedha bali iliandaa na kuwa mwenyeji wa Kukwaa la ununuzi wa umma nchi Wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki.Kongamano la mwaka huu 2021 limebeba Kauli mbiu isemayo "Maboresho ya mfumo wa ununuzi wa umma Nchini Tanzania :Mafanikio na changamoto zake"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad