Wizara ya Fedha yawakutanisha Wahariri wa vyombo vya habari kuwajengea uwezo kuhusu dhana ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi jijini Arusha - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 3, 2021

Wizara ya Fedha yawakutanisha Wahariri wa vyombo vya habari kuwajengea uwezo kuhusu dhana ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi jijini Arusha

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari wakati akifungua mafunzo ya siku 2 kwa wahariri hao kuhusu masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha.
Meza Kuu, ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba (katikati) wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiendelea wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu masuala ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.

Kamishina wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Dkt. John Mboya akizungumza wakati wa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.

Kamishina Msaidizi wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Bw. Bashiru Taratibu (kulia) akimsikiliza Kamishina wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Dkt. John Mboya wakati wa mafunzo ya siku 2 kwa wahariri hao kuhusu masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi yaliyofanyika leo juni 3,2021 katika ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha.


Baadhi ya wahariri wa Vyombo vya Habari na Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari wakati akifungua mafunzo ya siku 2 kwa wahariri hao kuhusu masuala ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha Juni 3, 2020Baadhi ya wahariri wa Vyombo vya Habari na Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo
 
Jumla ya miradi 41 imeandaliwa na kufanyiwa uchambuzi ambapo itagharimu kiasi cha shilingi trilioni 3.402, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Ndg. Emmanuel Tutuba amesema.

Ndg. Tutuba ameyasema hayo leo Juni 3, 2021 jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuwajengea uwezo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ubia kati ya serikali na sekta binafsi (PPP) katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Miradi 40, imeandaliwa na Mamlaka za Serikali kutoka sekta mbali mbali na mradi mmoja umeandaliwa na mwekezaji kutoka sekta binafsi.

Ndg. Tutuba alisema kuwa mpango huo una umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi miundombinu, Elimu, Afya, Mawasiliano, Maji, Michezo, Viwanda na biashara.

Ndugu Tutuba alisema kuwa serikali imeandaa programu hiyo ya PPP nchini ili kuwezesha sekta binafsi,kushirikiana na serikali kwa utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo, katika sekta mbali mbali ambazo ni

“Ndugu zangu mapato ya kodi peke yake hayatoshi kwa serikali kuweza kutekeleza na kuendeleza miradi yote hii,hivyo jitihada hizi zitachangia kujenga uchumi shindani,na wa viwanda kwa maendeleo ya watu ifikapo mwaka 2025/26”alisema Tutuba.

Kwa upande wake Kamishna wa PPP Dkt. John Mboya alisema kuwa faida nyingine ya kutumia utaratibu huu katika utekelezaji wa miradi na utoaji wa huduma ni pamoja na serikali kupata ubunifu,utaalamu na teknolojia kutoka kwa sekta binafsi na serikali kuhamasisha vihatarishi vya mradi vikiwemo vya kiufundi,kifedha na kiutendaji,ambavyo sekta binafsi ina nafasi nzuri ya kuvisimamia na kuongeza ubora wa huduma.

Alisema kuwa ili kuweka mazingira wezeshi ya kuishirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP Serikali iliamua kutunga sera ya PPP,ya mwaka 2009 na sheria ya PPP sura namba 103,na kanuni za PPP za mwaka 2020.

“Ndugu zangu ili kufikia azma ya kutekeleza Programu ya PPP na kwa kasi inayotakiwa ni jambo la msingi sana na kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana hiyo,ili wadau wetu washiriki kikamilifu kutekeleza sera na Sheria ya PPP,na elimu hii imekuwa ikitolewa ambapo kabla ya mwaka huu wa fedha jumla ya wadau 829 wamepatiwa elimu hii”alisema Dkt.Mboya.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad