HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 10, 2021

STARTIMES NA K4S WAHAIDI KUBORESHA FURSA KWA VIJANA

Mdau wa vijana pamoja na Muanzilishi wa Vituo vya habari nchini Joseph Kusaga akizungumza na Waandishi Wahabari Dar es salaam Mara baada ya kuzinduliwa kwa Tv3 yenye lengo la kutoa fursa kwa vijana wengi nchini huku akiwataka vijana kutengeneza Maudhui ya Kimichezo zaidi ili kuinua tasnia ya Michezo nchini
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa Uzinduzi wa Tv3 itakayopatikana kupitia King'amuzi cha Startimes itakayopatikana nchi ya Tanzania,Demokasia ya Kongo na Kenya



 Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

VIJANA Wahimizwa kukimbilia milango ya fursa hasa katika Sekta ya Michezo ili waweze Kunufaika pamoja na kuinua Michezo nchini.

Akizungumza na Waandishi Wahabari kwa Televisheni mpya ya Tv3 itakayoonekana kupitia King'amuzi cha Startimes Mkurugenzi wa  Clouds Media group Joseph Kusaga ambae pia ni Mdau Mkubwa kwa Sasa kwa vijana ,Mara baada ya Kufunguliwa amesema kutokana na Michezo kwa Sasa kupewa nafasi kubwa kwenye jamii inaonyesha iko wazi kuwa kupitia Sekta hiyo tunaweza kufungua Milango mingi ya ajira mbalimbali.

" Sehemu yoyote yenye Michezo lazima kuwepo kwa fursa mbalimbali zenye kulenga kukwamua vijana kiuchumi hivyo Mimi Kushirikiana na Startimes tumezindua rasmi Tv3 yenye Maudhui ya Michezo hasa ya Nyumbani ili kujitangaza zaidi ."

Hata hivyo Kusaga amesema ana lengo la dhati bado kuendelea kusaidia vijana katika Soko la ajira hasa katika tasnia ya habari na Michezo kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kwa jinsi gani Startimes wanavoendelea kuboresha huduma zao kwa kuwapatia wateja wao vitu vizuri na vyenye kukata kiu kuanzia Michezo, Filamu pamoja na tamthilia kwa Lugha ya Kiswahili.

"Tunaendelea Kukuza na kuendeleza Lugha yetu ya Kiswahili hivyo utaona upo umuhimu wa kuwepo Kampuni ya Startimes ili kupitia Burudani kunaweza kuwepo na Kuboresha Lugha yetu yani kinyumbani zaidi."

Malisa amesema Tv3  itapatikana kwenye Lugha ya Kiswahili ambapo Maudhui yake ni ya Kimichezo zaidi japo kutakuwepo na reality show pamoja na tamthilia.

"Tv3 kwa Sasa itatoa nyanja ya kutangaza vitu vilivyopo nchini kwetu Kimichezo na tamthilia hivyo itatupa fursa ya kutangaza utalii uliopo nchini kwetu hasa kukuza Lugha yetu ya Kiswahili."

Meneja Masoko wa Kampuni ya Ulinzi K4S Biko Scanda amehaidi Kushirikiana na Kampuni ya Startimes kidhati ili kuhakikisha Hali ya kiusalama zaidi katika Michezo.

"Kampuni yetu imekua Miongoni mwa Wadau wa Michezo hasa Mchezo wa ngumi na kuhakikisha ulinzi una imarika zaidi."

Tunawapongeza Sana Kampuni hiyo kwa kuendelea kutoa fursa za ajira mbalimbali kwa vijana kwani kuna baadhi ya vijana wengi wanajiingiza kwenye vitu vinavyohatarisha maisha yao na kupelekea kuwa vibaka.

"kwahiyo  kupitia K4S pamoja na Startimes tunazingatia kuendelea kutoa fursa za ajira zaidi na tunategemea Mechi ya ufunguzi wa Euro 2020 kesho katika uwanja wa Zakhiem tutaimarisha ulinzi wa kutosha" .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad