Na Amiri Kilagalila,Njombe
Muungano
wa wakulima wa zao la chai kupitia vyama vya ushirika MVYULU tarafa ya
Lupembe mkoani Njombe wamekubaliana kusitisha mgomo wa uchumaji wa
majani ya chai uliodumu kwa mwezi mmoja na kukubaliana kurejea shambani
hapo kesho April 12 mara baada ya makubaliano ya ulipwaji wa madeni yao
zaidi ya Bil 1 kutoka kwa wawekezaji wa viwanda vya Ikanga na Igombola.
Mbunge
wa jimbo la Lupembe Edwin Swale amesema uamuzi huo umefikia mara baada
ya majadiliano kadhaa ikiwamo vikao vya mara kwa mara yaliokuwa
yakifanywa baina ya serikali,wakulima,uongozi wa vyama vya ushirika
pamoja na wawekezaji wa viwanda hivyo vya Ikanga na kiwanda cha Chai
Lupembe (Igombola)
“Tumefanya uamuzi huo mkubwa tukiwa
tumekubaliana kwamba kuanzia sasa hatutasubiri wakulima kukaa zaidi ya
miezi miwili bila kulipwa tena,kwa hiyo kwenye ahadi na wawekezaji wa
Ikanga fedha ambazo wameahida kuwalipa wakulima wa chai mpaka mwishoni
mwa mwezi 4, basi tarehe 15 mwezi wa 5 tunakutana kuthibitisha”alisema
Edwin Swale
Amesema mgomo wa kuchuma chai ulianza March mbili
kutokana na malalamiko ya wakulima hao kuto kulipwa stahiki zao ili
waweze kujikimu katika maisha
“Tulifanya uamuzi huo tarehe mbili
mwezi wa tatu kwamba wananchi wa tarafa ya Lupembe,tusitishe kuchuma
chai na tuzungumze kwanza kuhusu malipo,wakati tunafanya uamuzi ule
tulikuwa na madai ya miezi mitano ya kulipwa,na mpaka hivi
ninavyozungumza mwekezaji wa Ikanga amelipa fedha ya miezi 5 na anadaiwa
mwezi wa pili tu” aliongeza Edwin Swale Mbunge wa Lupembe
Ameahidi
kuzungumza na waewekezaji ili kuweka utaratibu mzuri wa ulipwaji wa
fedha za wakulima“Tunataka tuweke utaratibu mzuri ni lazima wakulima wa
chai walipwe kila mwishoni mwa mwezi fedha yao wanayostahili kulipwa na
niwahakikishie wananchi hii ndio kazi mliyonituma,niwahakikishie madai
ya mwezi wa pili yatalipwa na madai ya mwaka 2018 yatalipwa” Edwin Swale
Mbunge wa Lupembe akiwa kwenye mkutano na wananchi wa Lupembe
Vile
vile amesema wawekezaji wa kiwanda cha Igombola mpaka sasa ndio
waliobakiwa na madai ya muda mrefu ukilinganisha na madai yaliyopo kwa
wawekezaji wengine kutokana na kupunguza madeni yao.
“Wawekezaji
wa Igombola hali yao ni mbaya zaidi,kwasababu kuanzia mwezi wa 12,1,2
na 3 hawajawalipa fedha wakulima wa chai na ahadi waliyoitoa kwenye
kikao mpaka tarehe 26 mwezi huu watakuwa wamewalipa wakulima malipo
yote” Edwin Swale
Hata hivyo amewataka wakulima wa chai kuto
kukata tama na kilimo hicho na kuhamia katika kilimo kingine badala yake
waweze kujihusisha na kilimo kingine pia ili kuwa na uwanja mpana wa
kukuza vipato vyao
“Mlio kata tamaa ya kuchuma chai na kuamua
kwenda kupanda parachichi na miti,nawaombeni mfanye mambo yote,kwasabbu
unavyopanda parachichi na zenyewe zikawa nyingi,kuna siku soko
litaanguka kwa hiyo msitupe chai.Wajibu wangu na viongozi wengine
tutahakikisha wakulima mnalipwa kwa wakati” alisema Swale
Kutokana
na hali hiyo wamiliki wa viwanda hivyo wamesema kutokana na kufikia
makubaliano hayo pia ikiwemo kuchuma majani safi na yenye viwango
stahiki wapo tayari kukamilisha malipo kabla ya mwezi Mei huku wakulima
wakikubaliana kukutana Mei 15 ili kujadili utekelezaji wa makubaliano
hayo.
No comments:
Post a Comment