HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 12, 2021

ZAIDI YA VIJANA 48,000 WANUFAIKA NA KAMPENI YA KIJANA NI USAFI

 NA FARIDA SAIDY, MOROGORO.


Vijana wametakiwa kuzingatia tabia chanya za usafi katika maeneo hayo ikiwemo kunawa mikono,kutumia maji safi pamoja na kudhibiti kusambaa kwa taka ngumu katika maeneo yao hali itakayosaidia kutunza na kulinda mazingira.
 
Wito huo umetolewa  wakati wa kampeni ya KIJANA NI USAFI ambayo inalenga kuhamasisha tabia ya usafi kwa vijana wakitanzania inayosimamiwa na Shirika la Raleigh Tanzania chini ya ufadhili wa   shirika  la msaada wa Uingereza( UKAID).
 
Kampeni hiyo itakayodumu ndani ya miezi 6 inawalenga vijana wa wakike na kiume wenye umri wa miaka kati ya 15-35,ambapo inatarajia kufikia zaidi ya vijana 48,000 katika mikoa ya minne ambayo ni Iringa,Morogoro,Dodoma na Dar es salaam. 
 
Akizungumza katika kampeni hiyo Mratibu wa Mradi,Bwana Augustino  Dickson amesema kampeni hiyo katika Manispaa ya Morogoro itajikita katika itahimiza matumizi ya maji safi na salama,na kuitaka jamii kuacha kuishi kwa mazoea.
 
Hata hivyo ameongeza kuwa Mkoa wa Morogoro unaathiwa na Magonjwa ya mlipuko ya mara kwa mara ya kiwemo mlipuko wa ugonjwa wa  Kipindupindu hali ambayo inatokana na  jamii kutotumia maji safi na salama.
 
Aidha ameongeza kuwa kampeni ya KIJANA NI USAFI itaendelea kulenga kundi la vijana kwa sababu vijana ndio kundi lenye idadi kubwa ya watu Nchini, huku akiongeza kuwa vijana wanaweza kuwa wakala wa mabadiliko chanya katika jamii endepo watajengewa uwezo kuhusu elimu ya mazingiara. 
 
Katika kampeni mafunzo mbalimbalia ya namna ya kuhifadhi maji safi na salama yametolewa kwa wananchi,huku wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakilishukuru Shirika la Raleigh Tanzania kwa kuwapatia elimu ya mazingira.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad