

Uzinduzi
wa Kampeni uliofanyika hapo jana Septemba 13 katika kitongoji cha
Mdaula Chalinze uliweza kuongozwa na mgeni rasmi ambae ni Mgombea nafasi
ya Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Ridhiwani Kikwete,ambae
aliweza kunadi sera zake kwa kuhakikisha jimbo la Chalinze linabaki
mikononi mwake kwa kuhitaji wananchi wamachagua yeye ili aweze
kuendeleza maendeleo katika Jimbo hilo.

Mbali
na hapo alipanda aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ulanga katika Mkoa wa
Morogoro ndugu Goodluck Mlinga na kutema cheche zake za kuhakikisha
anaunga mkono juhudi za chama chake cha mapinduzi nchi nzima kinapata
ushindi kuanzia Madiwani, Wabunge mpaka Mh. Dkt John Pombe Magufuli kwa
kupata ushindi mkubwa Katika kinyang'anyiro cha kiti cha urais, hali ya
kuwa ndugu Mlinga amepoteza nafasi ya kugombania ubunge kwa awamu hii.



No comments:
Post a Comment