MAENDELEO YA UJENZI WA HOSPITALI YA UHURU CHAMWINO YAIKUNA AIRTEL TANZANIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 14, 2020

MAENDELEO YA UJENZI WA HOSPITALI YA UHURU CHAMWINO YAIKUNA AIRTEL TANZANIA

 


Muonerkano wa Jengo la Hospitali ya Uhuru iliyopioWilayani Chamwino Mkoani Dodoma, ambao umekamilika kwa asilimia 87 na unatarajiwa kumalizika Oktoba mwaka huu. 

Mhandisi wa Ujenzi wa jengo la Hospitali ya Uhuruiliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, Bw. Girimu Kanansi (wa pili kulia) akimuongozaAfisa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia)alipotembelea Hospitali hiyo kuangalia maendeleo yake, ikizingatiwa fedha zamradi huo zilitolewa na Mbia mwenza wa Air tel Tanzania ambaye ni Bharti Airtel ya India kiasi cha Sh. bilioni 2.3.
Mhandisi wa Ujenzi wa jengo la Hospitali ya Uhuruiliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, Bw. Girimu Kanansi (kushoto) na AfisaMawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia), wakiwakatika picha ya pamoja na watumishi wa Kampuni ya Airtel Tanzania, baada yakutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo.

Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Bw.Jackson Mbando (kulia), akielekeza jambo alipotembelea moja ya Duka la Kampunihiyo lililofunguliwa jirani na linapojengwa jengo la Hospitali ya Uhuru MkoaniDodoma, ambapo Kampuni hiyo inamchango wake katika ufanikishaji wa mradi huo.


Mhandisi wa Ujenzi wa jengo la Hospitali ya Uhuruiliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, Bw. Girimu Kanansi (kushoto) akielezakuhusu ukamilishaji wake ambapo unatarajiwa kumalizika Oktoba mwaka huu. Kuliani Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando 
 
====  ===== = =======  ==========

Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino MkoaniDodoma umekamilika kwa asilimia 87 baada ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuzielekezatakribani Sh. bilioni 2.3 zilizotolewa na Kampuni ya Bharti Airtel ya Indiakujenga Hospitali hiyo.

Hayo yalibainishwa na Mhandisi wa Ujenzi wa jengo laHospitali ya Uhuru, Bw. Girimu Kanansi, wakati Afisa Mawasiliano wa AirtelTanzania, Bw. Jackson Mmbando, alipotembelea hospitali hiyo kuangalia maendeleoya ujenzi wake, Mkoani Dodoma

Bw. Kanansi alisema kuwa jengo hilo lililokamilika kwaasilimia 87 linajengwa kwa weledi mkubwa na Kampuni ya Suma JKT kupitia vijanawazalendo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kinyume na awali ambapo majengomakubwa kama hayo yalikuwa yanajengwa na kusimamiwa na wageni kutoka nje ya nchi.

“Kazi inayoendelea ni kutengeneza sakafu, kuwekamifumo ya umeme na kuskimu kuta, hivyo ninaishukuru Serikali ya Awamu ya Tanona Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel kuona umuhimu wa kupeleka huduma za Afyakaribu na wananchi hususani mkoani Dodoma ambako ndio makao Makuu ya nchi”,alieleza Mhandisi Kanansi.

Alisema kuwa Jengo hilo lilitarajiwa kukamilika mwezimei mwaka huu, lakini ilishindikana kutokana na changamoto ya msimu wa mvuakali ambao ulisababisha kutokuwa na mazingira Rafiki ya kusafirisha vifaakwenda eneo la ujenzi.

Aidha kutokana na hali hiyo Mkandarasi aliombakuongezewa muda, ambapo anatarajia kukamilisha ujenzi Oktoba mwaka huu iwapohakutakuwa na changamoto yeyote itakayojitokeza ikiwemo ya kutofika kwa vifaavya ujenzi kwa wakati.

Kwa upande wake Afisa Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Bw. Jackson Mbando, alisema kuwa Kampuni yake imekuwa na utaratibu wakutembelea eneo hilo la ujenzi ili kuona maendeleo yake kwa kuwa ni sehemu yakufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani miradi ya Afya ikiwemoHospitali ya Uhuru ambayo kupitia Mbia mwenza Bharti Airtel ya Tanzania ndio iliyotoa kiasi cha Sh. bilioni 2.3 kwa Serikali ambayo ilizielekeza katikaujenzi wa hospitali.

Alisema Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kutambuauhitaji wa huduma ya Mawasiliano, tayari imefungua maduka manne WilayaniChamwino likiwemo eneo la Hospitali ya Uhuru ambayo yataendelea kutoa hudumaikizingatiwa kuwa baadaya ya hospitali kuanza kufanya kazi huduma za fedhazitahitajika.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa Kampuniya Airtel Tanzania ikitoa Gawio kwa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha naMipango, Bw. Doto James alisema kuwa, Serikali ya Tanzania ilianza uchunguzi waumiriki wa Airtel Tanzania na baadae kufanya mazungumzo na Kampuni mama yaBharti Airtel ya India kuanzia mwaka 2018 na kufanikisha Serikali kumiliki asilimia 49 ya hisa za kampuni hiyo.

Alisema makubaliano hayo yaliyosababisha kunufaika kwapande hizo mbili ndiyo yalimfanya Mwenyekiti wa Bharti Airtel ya India, Bw.Sunil Mittal kutoa Sh. bilioni 2.3 kwa Serikali ikiwa ni shukrani kwa kuanzamakubaliano mapya yenye tija.

Katibu Mkuu Bw. Doto James, alisema kuwa Serikaliiliona vema fedha hizo zipelekwe kujenga hospitali ya Uhuru Mkoani Dodomaambayo inatarajiwa kumalizika mwezi Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad