WATUMISHI wa
Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kulinda mali za umma kama za kwao
binafsi ili ziweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
Maelekezo
hayo yametolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof.
Sifuni Mchome ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa
Wizara hiyo wakati akifungua mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro jijini Arusha.
“Watumishi
wote tunatakiwa kulinda mali za umma kama za kwetu binafsi na kuzitumia
kwa uangalifu mkubwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu”Alisema Prof.
Mchome
Aidha,
Prof. Mchome aliwaasa watumishi hao kuwa waadilifu kwa kutokunywa pombe
wakiwa kazini, madereva wasibebe abiria njiani wanapokuwa safarini, pia
watumishi wasiondoke na vifaa vya ofisi kwenda navyo nyumbani.
Mbali
na hayo, Prof. Mchome alizitaka Idara na Vitengo katika Wizara hiyo
kuwa na utaratibu endelevu wa kufanya vikao vya ndani mara kwa mara ili
kubaini na kutatua changamoto zilizopo ndani ya Idara na Vitengo na
kuepuka malalamiko kutoka kwa watumishi wa chini.
Alisema
,“Idara na Vitengo viwe na utaratibu endelevu wa kukaa vikao vya ndani
ili kujua na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya Idara na
Vitengo vyenu”.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Amon Mpanju
aliwaeleza watumishi ambao ni wajumbe wa baraza hilo kurudi kwenye
misingi ya utumishi wa umma na kuvaa ipasavyo kwa kuzingatia waraka wa
mavazi uliotolewa na Manejimenti ya Utumishi wa Umma.
“Watumishi
mnatakiwa mrudi kwenye misingi ya utumishi wa umma kwa kuzingatia
waraka wa mavazi uliotolewa na menejimenti ya utumishi wa umma na sio
mtumishi kuvaa mavazi yasiyostahili kwenye utumishi wa umma”, alisema
Naibu Katibu Mkuu huyo.
Katika
mkutano huo wajumbe walipata nafasi ya kusikiliza mada mbili ambazo ni
haki na wajibu wa mjumbe wa baraza la wafanyakazi pamoja na wajibu wa
chama cha wafanyakazi katika baraza la wafanyakazi na mahala pa kazi
iliyotolewa na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Manyara Bw. Samwel Said na mada
ya pili ilikuwa ushirikishwaji wa wafanyakazi iliyotolewa na Afisa kazi
Mkuu Mfawidhi Mkoa wa Manyara Bw. Perfectos Kimaty.
Awali
kabla ya kuanza kwa mkutano huo wajumbe walipata nafasi ya kuchagua
Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi kwani waliokuwepo wamemaliza muda
wao. Katika uchaguzi huo Bi Basuta Milanzi alichaguliwa kuwa Katibu wa
Baraza hilo baada ya kumzidi mshindani wake Bw. Felix Chakila ambaye
alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi.
Mbali
na kikao hicho, wajumbe walipata nafasi ya kufanya utalii wa ndani kwa
kutembelea hifadhi ya Ngorongoro na kujionea vivutio vilivyopo katika
hifadhi hiyo ikiwemo mchanga unaohama.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (wa pili
kushoto) ambaye ni mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi la wizara hiyo
akiongoza mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro.Wajumbe
wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika
picha ya pamoja na Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt.
Freddy Manongi baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa mbele ya mchanga unaohama katika Hifadhi ya Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment