Na Woinde Shizza, Michuzi Tv ARUSHA
WANAHABARI
wametakiwa kutumia kalamu zao katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa
ulaji wa mbogamboga kwa ajili ya uboreshaji wa afya zao ili kuweza
kuleta mabadiliko chanya katika nchi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika hitimisho la semina ya waandishi wa
habari iliyofanyika Tengeru jijini Arusha Mkurugenzi wa world vegetable
centre Gabriel Rugalema alisema kuwa waandishi ndio watu muhimu katika
kufikisha habari kwa haraka zaidi kwani wameonekana ni watafiti katika
mambo mbalimbali ya kijamii.
Rugalema
alisema sifa za mwandishi bora ni yule ambaye ataandika habari zenye
weledi kwa kudodosa na kuchambua kwa umakini habari hiyo kwa sababu
unaweza ukapewa habari ambayo haijakamilika na kutokuaminika.
"Kutokana
na warsha hii mtaongeza ubora wa kazi zenu Katika kuandika habari za
mada na tasnia ya mboga mboga kwani mwandishi bora anasifa ya kuwa
mtafiti, mchambuzi, mtashi na mwepesi wa kujifunza, sifa hizi zinatufaa
sana katika sekta ya mbogamboga alisema mkurugenzi huyo". Alisema Rugalema
Masunga
na Hilda Kinabo ni baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo
hayo walisema bado tanzania kuna ukuaji mdogo wa kilimo hicho tofauti na
mataifa mengine ikiwemo ulaji wa mboga mboga huku ikiwalazimu kutoa
elimu kwa jamii na umuhimu wa kilimo hicho.
Aidha
wamelishukuru shirika hilo kwa kutoa mafunzo hayo kwa kuwaelimisha
wakulima kutoka kwenye kilimo cha kizamani na kuingia cha kisasa na
kujifunza teknolojia ya udongo kwa ajili ya kuoteshea miche kwani ni
wakati wa wakulima kuamka na kuja kujifunza katika kituo hiki.
"Tumejifunza
kilimo cha kimkataba ambacho kina faida kubwa kufanya mkulima anaingia
shambani akiwa tayari amelifahamu soko sasa ni muda wa kutoa elimu kwa
wakulima alisema kinabo". Alisema Rugalema

Mkurugenzi
wa world vegetable centre Gabriel Rugalema akuonyesha waandishi wa
habari namna ya kuzuia wadudu washambuliao mazao kwa kutumia mifuko ya
lailoni.

mkulima
wa vitunguu ambaye pia Ni mkulima anaezalisha Miche ya aina mbalimbali
ya mbogamboga Alfred Lukumay akionyesha waandishi wa habari vitunguu
alivyovilima Mara baada ya kupewa elimu ya kilimo Cha mbogamboga na
shirika la World Vegetables center lililopo Tengeru mkoani Arusha juzi.
No comments:
Post a Comment