WATAFITI WAASWA KUJIKITA KWENYE TAFITI ZA DAWA ASILI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 24 October 2019

WATAFITI WAASWA KUJIKITA KWENYE TAFITI ZA DAWA ASILI


 Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Khadija Malima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Profesa Mohammed Sheikh na Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Taasisi ya Dawa asili, Dk. Khadija Malima. 
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi na Utafiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Profesa Mohammed Sheikh aikungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mtafiti Mwandamizi wa utafiti wa Mradi wa Fellow, Dk. Francis Machumi na katikati ni Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Khadija Malima. 

 Mkurugenzi wa Utafiti wa tiba asili, Joseph Otieno akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Profesa Mohammed Sheikh na Mtafiti Mkuu Kiongozi waTume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Khadija Malima. 

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
KUNA haja ya kuwekeza katika tafiti za ya dawa asilia nchini kwani Tanzania inamalia asili nyingi ambazo zitaweza kuimalisha afya ya kila mtu.

Hayo yamesemwa na Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Khadija Malima jijini Dar es Salaam leo wakati akingumgumza na waandishi wa habari ikiwa ni kuelekea mkutano wa mabaraza ya kitafiti utakaofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 11 hadi 15 unaondaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

"Ili kuhakikisha dawa asilia ni salama kwa binadamu, dawa hizo zinaweze kutibu na kuondoa matatizo ya magonjwa, dawa hizo zinatakiwa kufanyiwa utafiti na zitengenezwe ka kiwango cha hali ya juu na kwauwingi".

Khadija Amesema kuwa viwanda vikishiriki katika utafiti wa dawa asilia tuweze kupata dawa na kufungua soko la dawa asilia kwa nchini za Afrika mashariki na katika na nchi za kusini mwa jangwa la sahara.

Hata hivyo amesema kuwa tunaweza kujikita katika matumizi ya fedha za uuma kwaajili ya kwaajili ya kufanya tafiti ambazo zitatupatia dawa za asili lakini sio lazima ziwe zifikie kiwango cha vidonge kwani hiyo itachukua miaka mingi, lakini tukitumia maliasili  tuliyokuwa nayo tunaweza pia kuwekeza ili kujiletea maendeleo.

"Ili kuhakikisha hizo dawa ni salama kwa binadamu, ziweze kutibu na kuondoa matatizo ya magonjwa,zinatakiwa zitengenezwe kwa kiwango cha hali ya juu na kwa uwingi".

Hata Hivyo Mkurugenzi wa taasisi ya dawa asili, Joseph Otieno amesema kuwa biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza ni kwenye kitengo cha dawa asili kwani dawa huzi zinatafutwa na nchi za nje ikiwepo Marekani, Uholanzi, ujerumani, China na Kolea.

" Watu hawa wanakuja hapa Muhimbili katika Taasisi ya tiba asili wakihitaji tuweze kushirikiana nao ili waweze kujua dawa zinazotokana na miti dawa zinazoweza Kuendelezwa ili kupambana na maradhi yanayoongezeka duniani ambayo yamekuwa sugu na hayawezi kutibika kirahisi kwa dawa ambazo tayari zimevumbuliwa".

Otieno amesema kuwa Tanzania inamiti zaidi ya elfu 12 lakini kati ya hiyo zaidi ya asilimia 25 imesharekodiwa  kwamba ni ya dawa lakini kinachokosekana ni utafiti ambao unahusisha waganga wa asili, kuungwa mkono na serikali kuhakikisha kwamba hii miti inafanyiwa utafiti kwaajili ya kutibu magonjwa yanayotusumbua.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad