Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
ameziagiza Halmashauri za Miji pamoja na watu wenye mashamba makubwa
wahakikishe wanawalipa fidia Wananchi wote ambao hawajalipwa kwa muda
mrefu tangu kufanyika kwa tathmini kwani wananchi wengi wamekuwa
wakiishi ndani ya mashamba yao kwa muda mrefu na wakiamishwa hawalipwi
fidia zao kwa miaka mingi na wengine kuondolewa bila kulipwa kabisa.
Waziri Lukuvi meyasema hayo alipofanya ziara Wilayani Handeni Mkoani
Tanga wakati wa kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa Soko la
zamani Chanika maarufu Nyerere Squre Katika mkutano huo Waziri wa
Ardhi aliongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo Godwin Gondwe akiwa pamoja na
Mbunge wa Jimbo la Handeni Omari Abdallah Kigoda na watendaji
mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Kupitia kampeni yake ya "FUNGUKA KWA WAZIRI" Lukuvi amesikiliza
kero za ardhi za wananchi zaidi ya 200 wa wilaya ya Handeni
zilizowasilishwa kwake. Kampeni hiyo iliyoanza saa 4 asubuhi hadi saa
12 jioni ambapo wakazi wengi wa mji huo wamelalamikia suala la kulipwa
fidia ndogo au kutokulipwa fidia zao kabisa.
Lukuvi amesema Halmashauri nyingi zimekuwa na pupa za kupanga
viwanja bila kuwalipa wananchi fidia na hata ikitokea wakalipa fidia
basi fidia itakuwa ndogo sana kwani kwa kufanya hivyo kutazidisha
migogoro mingi ya ardhi isiyo ya lazima, hivyo amezitaka halmashauri
kupitia upya madai ya wananchi na kuwalipa stahiki zao.
”Kwa kuwa hapa sasa mashamba mengi ya mji huu yamegeuka kuwa ni miji,
lazima hawa watu muwafidie viwanja zaidi kuliko pesa kama wanataka
pesa basi wauze wenyewe hivyo viwanja, hamuwezi kuwapa shilingi
milioni tatu wakati nyinyi mnauza viwanja milioni kumi. Kumekuwepo na
unyang’anyi na kuwalazimisha watu kupima viwanja kwa fidia kidogo. Na
kwa mujibu wa sheria ya fidia kama hujamlipa mwananchi kwa miaka zaidi
ya miwili basi inatakiwa ufanye tathmini upya”.
Hata hivyo Lukuvi ameshangazwa na wingi wa migogoro ya Ardhi ambayo
ilikwisha patiwa ufumbuzi wake na mingine ilikwisha tolewa hukumu na
Mahakama lakini cha kushangaza bado wananchi wanacheleweshewa haki zao
hivyo kuwaamuru Maafisa ardhi kuhakikisha wanashughulikia swala hilo
haraka iwezekanavyo kwani asingependa kuona swala hilo likijirudia
tena.
Lukuvi amesema kuwa amebaini 90% ya Wananchi wa Handeni hawana
uwelewa juu ya hatimiliki ya ardhi zao wanazomiliki kwani ameshangazwa
sana kuona wengi wao hawafahamu mipaka ya maeneo yao hali inayopelekea
kuzuka kwa migogoro ya mipaka hivyo amewaasa wananchi kuyafatilia
maeneo yao na kuyapatia hati miliki ili kuyalinda na wavamizi kwani
Hati ndio kielelezo namba moja kinachotambulika kisheria.
"mimi kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ipo migogoro
ambayo nina uwezo wa kuitafutia ufumbuzi kutokana na mamlaka
niliyonayo na ndio maana nimeamua kuwa na kampeni ya Funguka kwa
Waziri ili kusikiliza kero mbalimbali za Ardhi lakini hii migogoro ya
mtu na mtu inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi ndani ya ofisi zenu za ardhi
au wilaya" Amesema Waziri Lukuvi.
Hata hivyo baada ya kusikiliza kero za wananchi Waziri Lukuvi ameahidi
kuanzisha Baraza jipya la Ardhi na Nyumba la Wilayani Handeni kwani
wananchi wamekuwa wakisafiri hadi Wilayani Korogwe kusikiliza mashauri
yao jambo ambalo limekuwa na ucheleweshaji wa kusikiliza na kutatua
kero za ardhi kwa wakati kwani ndio chanzo cha migogoro mingi Wilayani
hapo.
Aidha, akifunguka mbele ya Waziri Bi. Telessa Petro Gumbo ambae ni
mkazi wa Handeni amelalamikia uvamizi wa uliofanywa katika shamba lake
ambapo amemuomba Waziri Lukuvi kuingilia kati swala lake la
kutolulipwa fidia baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kulimega
eneo lake na kupitisha barabara hali inayomlazimu kulipwa fidia ya
eneo hilo.
Naye, Bi. Amina Ali Kiale ambae pia ni mkazi wa Handeni amemlalamikia
Waziri lukuvi kwa baadhi ya watendaji wa Ardhi ambao sio waaminifu
kushiriki katika vitendo vya kudhurumu ardhi kwa kuwacheleweshea hati
zao kwa muda mrefu wanapokuwa wanazifatilia.
Katika kutoa shukurani kwa Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Handeni
Godwin Gondwe amemshukuru Lukuvi kwa kitendo cha kuifanya programu
hiyo ya FUNGUKA KWA WAZIRI katika Wilaya yake ya Handeni kwani imeweza
kutatua migogoro ya ardhi iliyodumu muda mrefu na kuahidi
kushughurikia migogoro iliyobaki katika ofisi yake ya Wilaya.
Sharifa Mussa Mkazi wa kitongoji cha Chanika akimuonesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi madai yake ya fidia ya ardhi ambayo bado hayajalipwa wakati wa mkutano wa hadhara wa utatuzi wa kero za ardhi kwa wakazi wa mji wa Handeni katika uwanja wa Soko la Zamani Chanika maarufu Nyerere Square Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Amina Ali Kiwale Mkazi wa kitongoji cha Chanika akimuelezea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi madai yake ya fidia ya ardhi ambayo bado hayajalipwa wakati wa mkutano wa hadhara wa utatuzi wa kero za ardhi kwa wakazi wa mji wa Handeni katika uwanja wa Soko la Zamani Chanika maarufu Nyerere Square Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Sufian Sanyimina Mkazi wa kitongoji cha Chanika akimpa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi uthibitisho wa madai yake ya fidia ya ardhi ambayo bado hayajalipwa wakati wa mkutano wa hadhara wa utatuzi wa kero za ardhi kwa wakazi wa mji wa Handeni katika uwanja wa Soko la Zamani Chanika maarufu Nyerere Square Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya
Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.
No comments:
Post a Comment