HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 15 July 2019

KAMPENI YA PLASTIKI NOMA YALENGA KUHAMASISHA JAMII KUHUSIANA NA MADHARA YA TAKA ZA PLASTIKI

* Wananchi waombwa kushiriki usafi katika eneo la daraja la Salender Alhamisi Julai 18 mwaka huu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV 
UTAFITI wa madhara ya taka za plastiki katika bahari ya Hindi uliofanyika kuanzia Septemba 2018 hadi Sasa umekuja na kampeni kabambe ya kuelimisha jamii kuhusiana na madhara ya taka za plastiki katika bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mmoja ya watafiti hao ambaye pia  ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Vicensia Shule amesema kuwa utafiti huo ulifanyika katika maeneo kadhaa ya Pwani ya bahari ya Hindi likiwemo eneo la Salender jijini humo huku wakijiegemeza katika kuangalia aina na kiwango cha taka za plastiki zinazoingia au kutoka baharini pamoja na kuelimisha jamii ya tatizo hilo kwa kubuni mbinu za ukusanyaji na taka hizo.

Vicensia amesema kuwa  malengo mahususi ya utafiti huo yalilenga kupima taka za plastiki katika ukanda wa bahari jijini humo na kutafuta njia ya kurekebisha madhara hayo.

Amesema kuwa pia utafiti huo ulilenga kutathimini ufanisi wa sheria za nchi, sheria ndogondogo, sheria za kitaifa na kimataifa, kanuni na sera za taasisi zinazoingiza, kuzalishaji na kuagizaji vifaa vya plastiki ndani na nje ya nchi.

Vilevile ameeleza kuwa baada ya kufanya utafiti huo wameona ni vyema wakaja na kampeni hiyo ya kujenga uelewa na kuhamasisha jamii juu ya madhara yanayoletwa na taka hizo.

Kwa upande wake Dkt. Rose Massalu ambaye ni kiongozi wa utafiti huo amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kunategemewa kuzalisha ajira katika sekta mbalimbali huku wakiishukuru serikali kwa kukataza matumizi ya mifuko ya plastiki licha ya kuwepo kwa baadhi ya plastiki zikiwemo chupa za maji, mifuko ya pipi na kadharika.

Amesema kuwa kampeni hiyo itaenda sambamba na usafi utakaofanyika katika eneo la daraja la Salender na kwa kushirikiana na taasisi ya Baba Watoto Centre  watahusisha watoto na vijana 125 kutoka Manispaa zote ambao wamekuwa wadau wakubwa wa kufatilia shughuli za namna hiyo.

Kwa upande wake Dkt. Benjamini Ngatunga amesema kuwa katazo matumizi ya plastiki lililoanza Juni  na sheria juu ya katazo hilo wananchi wamelitii ndani ya mwezi mmoja pekee, jambo ambalo linatia moyo na kuona mwanga wa matumizi hayo ya plastiki kukoma.

Utafiti huo umehusisha watafiti wanne wakiwemo Dkt. Lydia Gaspare, Dkt. Rose Massalu, DKt. Benjamin Ngatunga na Dkt. Vicensia Shule.
 Mtafiti Kiongozi wa Utafiti wa madhara ya Takataka za Plastiki kwenye Bahari ya Hindi Dkt. Vicensia Shule akizungumza na waandishi habari kuhusiana Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha jamii madhara ya Plastiki itakayofanyika katika Ufukwe wa Selander jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Dkt.Benjamin Ngatunga akizungumza madhara ya Plastiki na nchi zilizochukua hatua ya kuzuia Plastiki jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad