HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 9, 2019

SERIKALI YA DENMARK WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO KATIKA KUBORESHA SEKTA ZA HAKI ZA BINADAMU NCHINI


Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Serikali ya Denmark kupitia ubalozi wake nchini wamesaini mkataba wa makubaliano wa kifedha katika mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubaliano hayo balozi wa Denmark nchini Mheshimiwa Einar Hebogard Jensen amesema kuwa mkataba huo umeelekezwa katika sekta tatu ambazo ni programu za utawala bora, upatikanaji wa haki na haki za binadamu.

Katika makubaliano hayo Serikali ya Denmark imetoa msaada wa Krona milioni 7 sawa na takribani dola za kimarekani milioni 1, 049, 776 huku tafiti zikionesha kuwa kwa mwaka 2018 walitoa jumla ya dola za kimarekani milioni 63.

Balozi Jensen amesema kuwa Denmark inaamini kuwa ili kufikia maendeleo lazima misingi ya uwazi, uwajibikaji na usawa wa kijinsia iwepo na wamekuwa na ushirikiano duniani kote na kupitia UNDP nchini Tanzania wamekuwa wakishiriki na kufanya kazi kwa pamoja katika  kuboresha shughuli za bunge, utawala bora pamoja na taasisi na vituo mbalimbali za haki za binadamu.

Aidha amesema kuwa watanzania wanazijua haki zao kwa kufuata sheria na hiyo ni kutokana na ukomavu wa demokrasia nchini.

Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Natalie Boulcy amesema kuwa Denmark ni moja kati ya nchi 10 zinazoshirikiana na kutoa msaada mkubwa kwaUNDP hasa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora na ulinzi.

Natalie amesema kuwa msaada utawafikia watu wengi zaidi hasa vijijini pamoja na  kusaidia sekta mbalimbali zikiwemo tume ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG) hasa katika kuwajengea uwezo, ikiwa ni pamoja na kuwezesha uchapishaji wa ripoti za haki za binadamu kwa kila mwaka na kuzimbaza kote nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na katiba na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali .

Pia msaada huo utaelekezwa katika makundi mbalimbali wakiwemo wanawake na watoto, ofisi ya Mwendesha Mashtaka mkuu wa serikali (DPP) kupitia Wizara ya sheria pamoja na vituo vya haki za binadamu na utawala bora.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely  wakikabidhiana mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely  wakisaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidmkatabaresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovel(kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam. Kulia ni mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovel(kulia) akimpa zawadi Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen  mara baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad