HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 8, 2019

TANZANIA KUPOKEA UGENI MZITO WA NCHI 16 KUTOKA SADC AGOSTI MWAKA HUU KUTOKA SADC

*Wafanyabiashara na wajasiriamali washauriwa kutumia fursa hiyo kutangaza biashara zao

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAFANYABIASHARA na wajasiriamali wametakiwa kutumia fursa ya kutangaza biashara zao kupitia mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) mkutano unaotarajiwa kufanyika nchini  tarehe 17 na 18 Agosti mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa kwa mara ya pili SADC wanatembelea Tanzania na hiyo ni baada ya taifa kupewa jukumu la kuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa umoja wa nchi za kusini mwa Afrika huku Rais Magufuli ambaye kwa sasa ni makamu mwenyekiti wa umoja huo atakuwa mwenyekiti kwa muda wa mwaka mmoja akipokea kijiti kutoka Namibia.

Profesa Kabudi amesema kuwa mkutano wa namna hiyo ulifanyika nchini mwaka 2003 na Rais wa awamu tatu Benjamin Mkapa alihudumu kama mwenyekiti kwa mwaka 2003/2004.

Amesema kuwa mkutano huo utaanza na maadhimisho ya wiki ya viwanda ya SADC  na kuwataka wajasiriamali na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo katika kujitangaza.

Aidha amesema kuwa majukumu ambayo mwenyekiti atakuwa nayo ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za kikanda, kusimamia mikutano ya kisekta kama vile afya na elimu.


Kwa upande wake naibu katibu mtendaji kutoka SADC Balozi Joseph Nourrice amesema kuwa wana amini katika ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja katika kuhakikisha nchi zilizopo katika umoja huo zina piga hatua.

Mkutano huo utakaokutanisha wakuu wa nchi 16 utaanza kwa mikutano ya ndani itakayoanza tarehe 6 Agosti kabla ya kuhitimishwa tarehe 18 mwezi huo na masuala mbalimbali nyeti na ya kidharura kama mafuriko na maafa katika nchi za Malawi, Zimbabwe na Msumbiji yatajadiliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad