HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 6, 2018

MANISPAA YA TEMEKE YAHUDUMIA WANANCHI MSIMU WA SABASABA


Na Zainab Nyamka, blogu ya jamii

HALMASHAURI ya Manispaa ya Temeke imepiga kambi katika viwanja vya sabasaba ikiwa na lengo maalumu la kuwahudumia wananchi katika msimu wa sabasaba na kuwataka wakazi wa Temeke wajitokeze kwa wingi ukizingatia maonesho hayo yanafanyika katika Manispaa yao.

Akizungumza na blogu ya jamii Afisa biashara wa Manispaa ya Temeke bi. Telphina Mbegu ameeleza kuwa katika msimu huu wa sabasaba wanatoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na leseni za biashara kwa wateja wapya na kwa wateja ambao leseni zao zimeisha muda wake wa matumizi.

Aidha ameeleza kuwa wanatoa leseni mbalimbali kama na ushauri kama  taratibu za ujenzi makazi, vileo na huduma mbalimbali za kibiashara.

Pia ameeleza kuwa kama Manispaa wanasikiliza kero na maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi na kutatua kero hizo zinazowakabili wananchi wa Manispaa hiyo.

Kuhusiana na kero walizopokea Mbegu ameeleza kuwa wananchi wengi wametoa kero kuhusiana na miundombinu hasa ya barabara, mifereji na takataka katika maeneo mbalimbali katika maeneo wanayoishi.

Pia ameeleza kuwa wanatoa elimu kwa wafanyabiashara wanaotaka kuanza biashara kwa kutoa elimu kuhusiana na upataji wa leseni kwa ajili ya biashara hizo.

Amewaomba wakazi wa Temeke na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili waweze kujifunza na kuelimika zaidi kupitia shughuli zinazofanywa na Manispaa hiyo.
 Afisa biashara wa Manispaa ya Temeke Telphina Mbegu akielezea huduma wanazozitoa katika banda liliopo ndani ya Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Afisa biashara wa Manispaa ya Temeke  Telphina Mbegu akimuelezea Jambo mwananchi aliyetembelea banda lao ndani ya Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad