HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 5, 2018

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AMTOLEA UVIVU MKANDARASI ANAYEJENGA MATANKI YA KUHIFADHIA MAJI DAR

*Ni baada ya kuchelewesha kukamilisha mradi uliotakiwa kumalizika mwaka 2017

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amemuagiza mkandarasi anayejenga matanki ya kuhifadhia maji na pampu na kusukumia maji kukamilisha mradi huo haraka hadi ifikapo mwishoni mwa Septemba mwaka huu

Amesema mkandarasi huyo Jain Irrigation system kutoka India  hadi sasa amekamilisha asilimia 87. 5 ya mradi huo ulioanza Machi mwaka 2016 na ulipaswa kukamilika Novemba mwaka 2017.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku tatu ya  kukagua  miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)  ambayo bado ipo kwenye utekelezaji katika maeneo mbalimbali jijini.

 Amesema mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji jijini ni wa muhimu na utagarimu Sh. bilioni 72.43 lakini inasikitisha mpaka sasa bado hajakamilisha.

 "Mradi huu ni muhimu sana kwani watanzania wengi hasa wananaoishi hapa jijini Dar es Salaam wanachangamoto kubwa ya maji,"amesema Mbarawa.

Amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa mradi huo ilikuwa ni kuhakikisha changamoto za maji kwa watanzania  zinakwisha lakini mkandarasi bado analeta shida.

Kutokana na  mapungufu hayo ya Mkandarasi, Waziri Mbarawa amemuagiza Meneja mradi huo, Anil Vitankar kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa haraka na pia amemuagiza mkandarasi huyo kuwepo kwenye eneo la mradi kwa saa 24, na kama akishindwa kumaliza mradi huo kwa wakati waliokubaliana ambao ni mwisho mwezi September basi hiyo ndio itakuwa mara yako ya mwisho kwa mkandarasi huyo kufanya kazi nchini.

Pia Serikali itahakikisha kwamba inamtoa kwenye usajili wa bodi ya wakandarasi.

" Tukifanya hivyo maana yake hautafanya kazi yoyote hapa Tanzania wala usijaribu kuomba tenda yoyote hapa Tanzania,"amesema.

Ameongeza  kama mkandarasi huyo hatatekeleza maagizo hayo basi Serikali itakunyang,'anya kibali chake cha kusafiria (Passport) ili kuhakikisha anafanya kazi na anamaliza.

Aidha, mradi huo pia utahusisha ujenzi wa vituo vinne vya kusukuma maji vilivyo na matenki ya kuhifadhi maji lita milioni tatu kila moja.

Pia utahusisha ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa 16, ununuzi wa transfoma na ufungaji wa njia za umeme wa msongo mkubwa.

Mradi huo utakuwa na kazi ya ununuaji na ulazaji wa mabomba ya ugawaji maji pamoja na ya kusambaza maji mitaani yenye urefu wa kilobits 477.

Waziri Mbarawa ameongeza  kukamilika kwa mradi huo siyo kwamba utapeleka maji kwa wananchi, bali hivyo ni vituo vya kusambazia maji.

"Amesema kuna mradi mwingine unaofadhiliwa na benki ya Dunia ambao utatoa maji kutoka kwenye hivyo vituo na kuwapelekea wananchi, ambao utagarimu Sh. Bilioni 100.

Katika ziara hiyo Waziri ametembelea mradi wa Bunju, Mabwepande, Salasala na Changanyikeni.
  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mbarawa (wa pili kulia), akikagua sehemu ya kuhifadhi vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa mifumo ya maji Dar es Salaam na Pwani,  unaosimamiwa na Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mbarawa, akitoka kukagua tenki la kuhifazia maji, Mabwepande, Dar es Salaam.
  Profesa Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kumpa maagizo mkandarasi wa Kampuni ya Jain Irrigation System kutoka nchini India  mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa mifumo ya maji Dar es Salaam na Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad