HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 29 June 2018

Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara

Na MwandishiWetu
Wakulima wa ufuta nchini wametakiwa kuachanana kilimo cha mazoe and kufanya kilimo biashara. Hasa katika kuongeza tija ya uzalishaji ili kukabiliana na changamoto wakati bei inaposhuka pamoja na kuweka kumbukumbu na kuwasiliana na wanunuzi kabla ya kulima mazaoyao. 

Hiyo ni pamoja na wakulima kujiunga katika vikundi rasmi au katika vyama vya ushirika ili kuweza kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha nchini ambapo serikali itawapatia dhamana kupitia vikundi hivyo.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba alisema hayo jijini Dar es Salaam katika kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilayaz a Bahi, Babati na Manyoni, kongamano hilo liliandaliwa na shirika la Farm Africa kwa kushirikiana na mashirika wenza ambayo ni INADES Tanzania, COSITA na MVIWATA. 

 “Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli mara kadhaa amekuwa akisisitiza umuhimu wa wakulima nchini kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kujikwamua kutoka kwenye kilimo kisicho na tija kwa sababu vyama vya ushirika vina fursa ya kupata dhama na ya serikali moja kwa moja,” alisisitiza.

Wadau wa walioshiriki kongamano hilo ni wakulima, wanunuzi wakubwa na wakati, halmashauri za Babati Manyara , Manyoni Singida, Bahi Dodoma na Kilwa, wakala wa mbegu ASA, wizara ya TAMISEMI, Viwanda   na wadau wengine ni Shirika la TOSCI watoa huduma kwa njia ya tehama ambao ni wawakilishi kutoka mashirika ya Esoko na Sibesonke .

Dkt.Tizeba alisema kwamba ni muhimu kuweka mifumo ya pamoja katika biashara na uendeshaji wa kilimo cha kisasa ili kuweza kuaminika na taasisi za fedha nchini na kuweza kupata mikopo ya uhakika na kufanya kilimo cha kisasa kwa manufaa ya nchini nzima.

Aliongeza kwamba kwa muda mrefu taasisi za kifedha nchini zilikuwa zinafikiria kwamba kilimo si biashara na kuacha kuwakopesha wakulima lakini kwasasa tunawataka kuanza kuwakopesha wakulima hasa kilimo cha ufuta .

“Ninapongeza baadhi ya benki nchini zimeanza kuwakopesha wakulima kwa mwaka jana benki ya CRDB ilikopesha wakulima kiasi cha Tsh 460 billioni,” aliongeza.

Alisisitiza kwamba wakulima wa tumbaku wamepiga hatua kubwa kwenye kilimo hicho kutokana na kuwa kwenye ushirika ambapo wanapata mikopo yao kwa haraka kutoka kwenye mabenki nchini, wakati huo huo wakulima hao wa tumbaku mwakani wanatarajia kuvuna tani 65 elfu. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikalisilo la kiserikalila Farm Africa Bw. Ryan Whalen alisema kwamba fursa zipo kwenye  zao la ufuta ila ni muhimu kwa wakulima kuwe mkazo katiki kuongeza tija.

Akitoa mfano alisema wakulima waliowezesha na shirikika la Farm Africa kufanya kilimo bora waliweza kuongeza uzalishaji kutoka kilo 92 hadi kilo 202 kwa ekari sawa na ongezeko la asilimia 54 ambalo lime changiwa na matumizi ya mbegu bora.

 Aliongeza kuwa kwa kipidi cha mwakajana pekee wakulima Babati, Bahi na Manyoni walizalisha na kuuza ufuta wenye thamani zaidiya Tsh. Bilioni 10. Pia alioneza kusema fursa bado ni kubwa ya kuongeza pato kwa Mkulima kutoka tsh264,600 ya sasa hadi kufikia tsh. 515,000 kwa ekari. 

“Na kama wakulima hawa watajikita katika kuongeza uzalishaji na tija katika zao la ufuta wataweza kupata zaidi  yaTsh. Billion 36.”alisema.

Aidha Meneja Mwandamizi wa Kuendeleza Program ya kilimo kutoka Farm Africa Bw. Tumaini Elibariki alieleza kuwa mradi huo ni wa kuendeleza mnyororo wa dhamani  zao la ufuta na ulikuwa wa miaka mitatu na umefikia wakulima zaidi ya 11,177 wa wilayaza Bahi, Manyoni na Babati na wastani wa kipato chao kimeongezeka kutoka Tshs 685,160 hadi Tshs 984,244 kwa kaya kwa mwaka. 

Bw. Tumaini aliongeza kwamba ili kilimo cha ufuta kiwe na tija ni lazima wakulima wakubali kubadilika na kushirikiana na wadau wote katika kuwekeza kwenye huduma muhimu hususani za ugani, pembejeo na maghala ya kuhifadhia mazao, kukusanya na kuuza kwa Pamoja ili kuwa na kilimo chenye faida kubwa.

Kwa upande wake mkulima wa ufuta kutoka Mkoa wa Singida, wilaya ya Manyoni kijiji cha Sasajila, Christina Ndahan alisema kwamba kilimo cha ufuta ni moja la zao bora kabisa ambalo linaweza kumtoa mkulima kwenye umasikini na kuachana na jembe la mkono kwenye kilimo.

“Jambo kubwa ambalo ni changamoto ni jinsi ya kuongeza tija katika mnyororo wa thamani kwenye zao hili kwa kupunguza madalali ambao wanafanya mkulima kutokujua bei elekezi kwenye soko,” alisema

Alifafanua kwamba mlolongo mkubwa wa kumfikia mnunuzi wa mwisho wa ufuta ndio moja ya changamoto kubwa kwa wakulima wa ufuta ambao mnyororo wa madalali wa zao hilo ni kikwazo.

“Kupitia zao la ufuta nimeweza kujenga nyumba, kununua bodaboda na kusomesha watoto wangu shule zabinafsi na kwa kweli kipato change kimepanda kutokana na zao hili na natoa wito kwa watanzania wenzangu kujiunga na kilimo hicho maana kinalipa,” alisema Bi Christina.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen kushoto aliyesimama  akifafanua jambo wakati wa wakati wa  kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta kutoka wilaya za Kilwa, Bahi, Babati na Manyoni na liliandaliwa na shirika hilo, kulia ni  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida Manyoni, Bw.Charles Fussi, wa pili kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki. 
 Meneja Mwandamizi wa Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki aliyeye simama akieleza jambo wakati wa  kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilaya za Bahi, Babati, Kilwa na Manyoni lililoandaliwa na shirika hilo, kulia kwake mwenye laptop ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen na wengine ni wadau wa zao hilo. 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba wa pili kulia akifafanua jambo wakati wa  kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilaya za Bahi, Babati na Manyoni na liliandaliwa na shirika la Farm Africa, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen, kushoto Meneja Mwandamizi Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki na wa pili kushoto Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida  Manyoni,Bw.Charles Fussi.
 Wadau wa zao la ufuta kutoka wilaya za Kilwa, Bahi, Babati na Manyoni wakiwa katika  kongamano la siku mbili la wadau wa zao hilo lililoandaliwa na shirika la Farm Africa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad