HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 30 April 2018

USHINDI DHIDI YA YANGA, MANARA AWASHUKURU MASHABIKI

 Assalaam Aleikum.

Salaam zangu za Mei Mosi

Kwanza sote tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma anaendelea kutupa uhai na uzima hadi siku ya leo.
Hakika pumzi hii ndio inatufanya tufurahi na kuhuzunika pamoja,pia ndio inayotufanya tuweze kuandika na kusoma maandiko mbalimbali ikiwemo andishi hili dogo

Jana pale uwanja wa taifa palifanyika mechi kubwa kabisa ktk ukanda huu wa Afrika Mashariki. Simba na Yanga zote za hapa jijini Dar.

Sio vyema kurejea kuwapa matokeo ila Alhamdulillah klabu yangu ya Simba imefanikiwa kushinda na kujisogeza karibu kabisa na ubingwa wa ligi kuu nchini

Nimeandika kujisogeza kwa kuwa bado hatujatwaa ubingwa.kwa sasa tunahitaji points tano tu ili tuweze kutawazwa ubingwa huu unaosubiriwa kwa hama na washabiki wote kote nchini

Kiukweli hzi points tunazohitaji tutazisaka kwa tahadhari zote na kwa kutambua kiu ya wanasimba.. tutaingia kwenye michezo ilobaki kwa nguvu kubwa na kwa umakini wa hali ya juu,sambamba na kuwaheshimu wapinzani wetu

Ukiachana na hayo nna vitu vwili very special nataka kuvisema hapa

Kwanza ni shukran kwa washabiki wetu..ktk maisha yangu yote nilioishi sijapata kuona washabiki kama wa Simba..
Ni watu wasikivu mno na wenye subira na upendo wa hali ya juu,ni watu wanaopenda futboll halaf ndio timu yao,wana ustaarabu uliopitiliza na wenye mapenzi yasio na shaka kwa klabu yao,

Kwenye ustaarabu huwa natolea mfano wa kitendo cha kutoa back pass kwa mchezaji Hassan kesi wakati akiichezea Simba kwa Donald Ngoma wa Yanga na kutufunga goli la kizembe zaid ktk historia ya derby hii

Inawezeka kabisa ilikuwa ni bahati mbaya,ila kilichostaajibisha muda mchache ujao mchezaji huyo alihamia Yanga tena kwa maneno mabaya ya dharau na kebehi..naapa Wallah kitendo kile ingekuwa kwa wenzetu kessi angeuhama mji huu na kurudi Morogoro (tamka Mrogoro)

Ustaarabu wa watu wa Simba unadhihirishwa na uvumilivu wao ktk miaka minne ya nyuma kwa vitendo lukuli dhidi ya klabu vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya viongozi wa mamlaka za Soka,na hili c vema kulirejea kutokana na sababu za kibinadaam zaidi.

Hawa kwangu ni watu special ni watu ambao wamenirahisishia kazi yangu ya upashaji habari..washabiki hawa ni zaidi ya ndugu zangu ingawa wengi siwajui kwa majina na sura.

Na mfano hai ni mechi ya jana..ktk historia ya hz timu mbili haijapata kutokea washabiki kwenda uwanjani wengine wawe zaidi ya asilimia themanini. 
Yes jana imewezekana.nimewahamasisha wakahamasika nimewaaminisha wakaamini nimewaambia nyie ndio timu kubwa,bora na yenye fans wengi kupita zote nchini na jana wamelidhihirisha hilo kwa vitendo.

Hakika kama kuna tuzo ya washabiki bora nchini wanastahili kupewa Simba Sports Club.

Na kwa kupitia makala hii  niwashukuru sana washabiki wetu mmetuvika nguo na sisi hatutawaangusha msimu huu,mtapata mtakacho Inshaallah 

Jambo la pili nnalotaka kuandika ni kitendo cha beki na nahodha wa Yanga kelvin Yondan kumtemea mate mchezaji wetu Asante kwasi bila sababu yoyote na kama Tv yetu bora nchini Azam Tv ilivyootuonyesha jana

Mara baada ya kumalizika kwa mechi ya jana kila mshabiki aliyepata fursa ya kuongea na mm alilalamikia 'ushenzi 'ule.wapo walionipigia cm na wapo waliondika kwenye page yangu ya Instagram..ila niliumia zaid kuona hata kwasi mwenyew akimlalamikia meneja wetu kwa msg aliyotutumia jana usiku na kututaka management ya klabu ilichukulie kwa uzito mkubwa jambo hili

Yondan ni mchezaji mwandamizi nchini ni nahodha na kiongozi ndani ya uwanja na amecheza derby nyingi kupita wachezaji wote waliocheza jana,na haitegemewi mchezaji wa calibre yake kufanya uhuni wa aina ile.

Kumtemea mate mwanadamu mwenzio ni tusi kwa utamaduni wa taifa lolote lile duniani.ni dharau na ni ubaguzi ukizingatia aliyemfanyia ni raia wa Ghana.
Ni ushamba na fedheha kwa klabu yake na nchi kwa ujumla

Ni ulimbukeni na kujiona yy hawezi kufanywa lolote na mamlaka na kiukweli ni jinai pia inayofanyika ndani ya uwanja

Kwangu mm hiki ni kitendo cha hovyo kuwahi kukishuhudia ktk derby ya Simba na Yanga...tambua mm nimehudhuria zaidi ya derby 70 za miamba hii...
Sijapata kuona wala kusikia unyama wa aina ile uwanjani

Matarajio yetu kama klabu ni kuona hatua stahiki za kinidhamu zinachukuliwa dhidi yake tena kwa uharaka

Na kwenye hili hatutarajii kuona adhabu nyepesi za kufungiwa mechi mbili tatu..lazma itolewe adhabu kubwa itakayotoa fundisho kwa wachezaji wengine ili wasithubutu kufanya uharamia kama ule

Ikumbukwe adhabu ya Juma Nyoso iliotokana na udhalilishaji..
Hatuwapangii bodi na tff lakini pia hatutegemei huruma au kuangalia ukubwa wa timu na ktk hili hatutaandika barua tukiamini bodi na tff wana watu makini na watenda haki watakaoalichukulia jambo hili kwa uzito unaostahili.

Mwisho

Niwaambie tumejiandaa kisaikolojia kuwa mabingwa ila tusifanye sherehe yoyote kwa sasa..pia tunapiga marufuku kutengeneza jezi za Simba bingwa hadi pale tutakapofikisha points ambazo wengine wanaziona kwetu tu


Adiooooos

Haji Manara

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad