HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 30 April 2018

YANGA KUWAFUATA WAARABU MEI 03, YAJIPANGA KWA USHINDI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga wanatarajiwa kuondoka nchini Mei 03 kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger nchini Algeria.

Yanga iliyoingia katika hatua makundi ya kombe la Shirikisho baada ya kuwaondoa Welayta Dicha itashuka dimbani Mei 07 kupambana na USM Alger ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kundi D.

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana dhidi ya Simba kumalizika, Yanga sasa wanaweka nguvu zao zote kwenye mashindano hayo ili kuhakikisha wanazidi kufanya vizuri.

Mkuu wa Kitengo wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga Dismas Ten amesema kuwa kwa sasa nguvu zote wanaelekeza katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi yao ya kwanza.

Ten amesema kuwa Yanga wataondoka nchini kupitia Dubai na kisha kuelekea nchini Alger ili kuwahi kufika nchini humo pamoja na kuzoea hali ya hewa.

Yanga kwa sasa inayosimamiwa na kocha msaidizi Shadrack Nswajigwa imekuwa na matokeo sio mazuri toka kuondoka kwa kocha mkuu George Lwandamina kuachana na timu hiyo na michezo minne ambayo imesimamiwa na msaidizi wake ameshindwa kuwapa ushindi.
 
Ikumbukwe hivi sasa Yanga ndiyo timu pekee inayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ya kimataifa baada ya Simba kuondoshwa na Al Masry SC kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ilipangwa kundi moja 'KUNDI D' na timu za U.S.M Alger, Rayon Sports na Gor Mahia FC kwenye hatua ya makundi baada ya kuindosha Wolaita Dicha SC ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad