HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 11 April 2018

LIGI KUU WANAWAKE BARA HATUA YA NANE BORA KUENDELEA APRILI 21

Na Zainab Nyamka, Globu ya  jamii

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara hatua ya Nane bora inatarajia kuendelea Jumapili Aprili 21 kwenye viwanja tofauti.

Hatua hiyo ya Nane bora ambayo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) iliyokuwa kambini kujiandaa na mchezo wake wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake itaendelea katika mzunguko wa Tano.

Pia hatua ya nane bora inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ikishirikisha timu za Panama FC ya Iringa inayotumia Uwanja wa Samora, Evergreen Queens ya Dar es Salaam inayotumia Uwanja wa Karume, JKT Queens ya Dar es Salaam wanaotumia Uwanja wa Mbweni na Alliance ya Mwanza wanaotumia Uwanja wa Nyamagana.

Timu nyingine ni mabingwa watetezi Mlandizi Queens ya Pwani wanaotumia Uwanja wa Mabatini,Baobab ya Dodoma wanaotumia Uwanja wa Jamhuri Dodoma,Kigoma Sisters ya Kigoma wanaotumia Uwanja wa Lake Tanganyika na Simba Queens wanaotumia Uwanja wa Karume.

Huu ni msimu wa pili wa Ligi ya Wanawake kuchezwa ambapo katika msimu wake wa kwanza timu ya Mlandizi Queens ndio waliibuka na ubingwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad