HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 11 April 2018

RC SHINYANGA AWATAKA WAKAZI MKOA WA TABORA KUTUNZA , KULINDA MISITU ASILI

Na Tiganya Vincent
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack amewataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kutunza na kulinda mistu ya asili na miti inayopandwa sasa hivi ili ikuyafanya mazingira kuwa endelevu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema kama watafanya mchezo na kuacha baadhi yao watu waingie ndani ya mistu na kukatakata ovyo rasilimali za mistu upo uwezekano wa hali kuwa mbaya  na kukosa hata mvua kidogo zinapatikana hivi sasa kutokana na kutoweka kwa mistu.

Telack alitoa rai hiyo jana mjini Tabora wakati akifunga kongamano la siku la mazingira ambalo liliwahusisha wadau mbalimbali likiwa na lengo la kuweka maazimio ambayo yatasaidia katika kupambana na uharibifu na mistu.

Alisema kama wanataka kuona athari za uharibifu wa mazingira , wanatakiwa kwenda kuangali Shinyanga ilivyoathirika na ukataji ovyo wa miti katika Wilaya mbalimbali kama vile Kishapu.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa ni vema wananchi wakaungana na viongozi na wadau wengine kuwakemea wale wote wanaingia katika mistu na kukata miti hivyo hata bila ya kuwa na vibali vya viongozi.

"Sisi Shinyanga tumeamua kusimamia Sheria hakuna kukata mti bila kupata kibali ya Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya ...tukimkata mtu amefanya hivyo bila kibali tutamshughulikia kwa mujibu wa Sheria" alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema hairusiwi kukata mti mzima ili kupata nishati ya kupikia badala yake wananchi wanatakiwa kukata matawi kwa ajili ya kupikia na baada ya kupata kibali.

Alisema mtu atakayekutwa ameangusha mti mzima kwa kisingizio cha kupata kuni atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Mwanri aliwataka watendaji wa ngazi zote mkoani Tabora kuhakikisha wanasimamia Sheria zilizopo katika kulinda miti iliyopandwa na kulinda mistu yote ya hifadhi.

Naye Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma ya Mistu Tanzania(TFS) Valentine Msusa alisema kuwa kuanzia sasa Maafisa wote wa TFS hakuna kukaa Ofisi badala yake watagwanywa katika mistu mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na uharibifu .

Alisema ikikutwa katika msitu fulani kuna uharibifu Afisa anayesimamia msitu huo atawajibishwa kwa kuzembea na kupelekea watu kuingia ndani yake na kuharibu miti.

Aidha katika kikao wajumbe waazimia kuwa kila kijiji ni lazima kiwe na msitu wake na ulindwe .
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akifungua jana kongamano la siku moja la wadau mbalimbali la kujadili masuala ya kuboresha hali ya ulinzi na usalama mkoani humo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku wa mazingira uliofanyika jana mjini Tabora. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack  akisisitiza jambo wakati wa kufunga mkutano wa siku wa mazingira uliofanyika juzi(jana) mjini Tabora.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi na kushoto ni Mkiuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri. Picha na Tiganya Vincent

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad