HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 1 February 2018

MSANII WA NCHINI UGANDA RADIO AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki wa Nchini Uganda, Moses Sekibooga maarufu kwa jina la kisanii Mozey Radio afariki dunia

Mwanamuziki huyo alikimbizwa Hospitali ya Nsambya siku ya tarehe 23 Januari, 2018 baada ya kuanguka na kuvunjika shingo na fuvu la kichwa wakati akiwa kwenye ugomvi na mlinzi wa ukumbi mmoja wa starehe

Hata hivyo Hospitali hiyo haikuweza kumhudumua kutoka na kitengo cha wagonjwa mahututi kujaa ndipo msanii huyo alihamishiwa Case Clinic iliyopo Bungando Road JIjini Kampaka
Hapo jana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad