HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 15 January 2018

Johari Mussa, mshindi wa Milioni 10 Mlimani City.

MSHINDI wa Promosheni ya Mlimani City katika kipindi cha msimu wa siku kuu ya Krismass na Mwaka mpya ya fanya manunuzi Mlimani City na ushinde ijulikanayo kama “Mlimani City Grand Shopping Fest” amepatikana mwishoni mwa wiki mara baada ya kuchezesha droo kubwa na ya mwisho ambaye ni Johari Mussa mkazi wa Makongo juu jijini Dar es Salaam.

Johari aliibuka mshindi jana kajishindia vocha yenye thamani ya Shilingi milioni moja na zawadi zake tayari zimesha nunuliwa na ziko tayari kwa kukabidhiwa rasmi.
Johari aliibuka mshindi katika droo kubwa iliyohudhuriwa na mgeni rasmi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora aliwapongeza uongozi wa Mlimani City kwa ubunifu wa hali ya juu wa kuwajali wapangaji wao pamoja na wateja wanaofanya manunuzi Mlimani City na kuwaomba waendelee na Kampeni za ubunifu kama hizo kwani zinammfanya mpangaji na mteja ajisikie vizuri kuwa anathamani na mchango wake unathaminika afanyapo manunuzi yoyote Mlimani City.

Profesa Kamuzora alisema Serikari inatambua mchango wa Mlimani City na inauthamini sana kwani huduma bora na za kimataifa zitolewazo na Mlimani City sifa ni kwa Taifa pia.
Aidha pia aliwapongeza washindi 100 wote waliopatikana katika kipindi cha promosheni ya kila wiki kwa wiki tano mfululizo ambao walijishindia vocha yenye thamani ya Shilingi laki moja kila mmoja, lakini pia aliwapongeza washindi watano(5) waliojishindia vosha yenye thamani ya shilingi milioni moja kila mmoja na zaidi alimpongeza mshindi mkubwa, Johari Mussa mkazi wa Makongo kwa kuibuka mshindi wa vocha yenye thamani ya milioni kumi ambapo alitoa wito kwa washindi na ambao hawakushinda kuwa mabalozi wazuri wa Mlimani City.

Nae Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso aliwapongeza washiriki wote waliofanikwa kuingia kwenye ushindani wa kupata bahati ya kujishindia zawadi na kuwaomba wasikose kushiriki tena awamu nyingine. 
 Meneja Mkuu wa Mlimani City Mall, Pastory Mroso(kushoto) akimuonyesha Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora(katikati), zawadi za mshindi wa kwanza wa promosheni maalumu ya siku kuu ya Krissmas na Mwaka mpya zenye thamani ya Shilingi milioni kumi.Droo ya kumpata mshindi ilifanyika Mlimani City mwishoni mwa wiki.Kulia ni Oparasheni Meneja wa Mlimani City, Girish Kumar.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora(kashoto) akisoma kuponi ya mshindi wa kwanza wa promosheni maalumu ya siku kuu ya Krissmas na Mwaka mpya yenye thamani ya Shilingi milioni kumi.Droo ya kumpata mshindi ilifanyika Mlimani City mwishoni mwa wiki.Kulia ni Mwakilishi kutoka Gaming Board, Abdalah Singano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad