HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 20, 2017

UKAGUZI WA MABASI UBUNGO NI ENDELEVU KATIKA KULINDA USALAMA SAFARI ZA ABIRIA –KAMANDA SOLOMON

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo amesema kuwa ukaguzi wa basi katika kituo cha Ubungo ni endelevu ikiwa ni kulinda usalama wasafiri wanaokwenda mikoani na si vinginevyo.

Kamanda Mwangamilo ameyasema hayo leo wakati ukaguzi wa basi za mikoani katika kituo kikuu cha basi Ubungo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa katika kufanya ukaguzi pamoja na kuangalia wananchi wanasafiri kwa bei elekezi zilizotolewa na serikali kutokana na baadhi ya watu wa kupandisha nauli kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Amesema kuwa baadhi ya basi 10 zimetolewa namba za usajili kutokana na kubainika kuwepo kwa makosa ya kiufundi na baada ya kufanyiwa marekebisho watarejea na safari.

Kamanda Mwangamilo amesema kuwa kusitisha kwa basi lisifanye safari likiwa na abiria hakuna nia mbaya bali kuangalia usalama wananchi kuwa safari kuwa ya uhakika.

Nae Afisa Elimu wa Baraza la  Walaji  la Mamlaka ya Usafri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRACC), Nicholous Kinyariri amesema kuelekea mwisho wa mwaka kuna baadhi ya kampuni zinapandisha nauli hivyo lazima liangaliwe .

Kinyariri amesema kuwa  katika kipindi hiki wanataka ushirikiano kwa wananchi pale wanapoona kuna vitu vinakwenda nje ya utaratibu ili sheria ichukue mkondo wake.

 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akitoa maelekezo katika kwa askari wa usalama barabarani katika kituo kikuu cha basi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari wa kikosi cha Usalama barabarani  aking'oa namba ya usajili wa basi la kampuni ya Muro Princess baada ya kukutwa na makosa hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa abiria leo jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi wa Ukaguzi wa mabasi katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, Ibrahim Samwix akipata maelezo ya dereva wakati wakifanya ukaguzi wa basi la kampuni ya City Boy  leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akimpa maelezo Mkaguzi wa Ukaguzi wa mabasi katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, Ibrahim Samwix wakati ukaguzi mabasi katika kituo hicho.
 Mkaguzi wa Ukaguzi wa mabasi katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, Ibrahim Samwix akiingia kufanya ukaguzi basi la kampuni ya City Boy , leo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa kikosi cha Usalama barabarani  aking'oa namba ya usajili wa basi la kampuni ya City Boy baada ya kukutwa na makosa hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa abiria leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Elimu wa Baraza la  Walaji  la Mamlaka ya Usafri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRACC), Nicholous Kinyariri akizungumza na Michuzi TV katika kituo kuu cha basi Ubungo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad