HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 20 December 2017

WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA HUDUMA KATIKA KITUO CHA USULUHISHI (CRC)

 Daktari Mateu Innocent akimhudumia moja ya wateja waliojitokeza kwa ajili ya kupata huduma kwenye kituo cha usuluhishi (CRC) ikiwa ni katika mikakati ya kupinga na kudhibiti ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na kutoa huduma kwa elimu ya wananchi.

Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia ( CRC) kimejizatiti katika kusaidia kuleta uelewa kwa jamii kwa kwenda kutoa huduma kwenye maeneo mbalimali ikiwemo kuwa karibu zaidi na jamii.

Huduma hiyo iliyoanza kutolewa Desemba 11 na Kituo cha Usuluhishi –CRC, kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) imelenga kusogeza karibu na wananchi huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo hususani kwa wanawake na watoto wadogo.
Huduma hizo za pamoja zilianzia katika Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam na wananchi wengi waliweza kujitokeza ambapo awamu ya pili ilikuwa ni Kata ya Kawe.

Huduma zilizotolewa ni pamoja na msaada wa kisheria kwa waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, Ushauri nasihi na kuwepo kwa Dawati la Jinsia linalohudumiwa na Jeshi la Polisi, ustawi wa jamii  sambamba na huduma za kisheria kutoka kwa wanasheria.

Baadhi ya wananchi waliopatiwa huduma kituoni hapo walisema wanafurahishwa na huduma hizo muhimu kutolewa eneo moja jambo ambalo linawapunguzia mzigo na urasimu wanapoziitaji pia wameweza kupatiwa huduma kwa wakati na ikiwemo mashauri mengine kusikilizwa hapo hapo na kupatiwa ufumbuzi huku mengine yakienda mbele zaidi kisheria.

Daktari Matau Innocent amesema kuwa kituo cha usuluhishi kimeweza kuwasaidia wananchi wanaokutana nao kupata huduma kwa urahisi zaidi na pia inafanya wigo wa  huduma kuwa mkubwa sana. Matau amesema kuwa huduma wanazozitoa ni pamoja na upimaji wa maambukizi ya VVU, ushauri nasaha ukiachana na masuala ya ukatili wa kijensia hususani kwa wanawake na watoto.

Huduma za usuluhishi kutoka katika kituo cha CRC zimeweza kuleta hamasa kubwa kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali  wanaishi ndani ya vitendo vya unjanyasaji lakini wanashindwa kujitokeza kutokana na umbali na urasimu uliopo katika kupata huduma hizo, hivyo kuwa na huduma hizo karibu zinaweza kusaidia katika kutoa elimu na kupunguza ukatili wa kijinsia na masuala ya kijamii kwa ujumla.

Hivi karibuni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi –CRC, Bi. Gladness Munuo kilichopo chini ya TAMWA, aliishauri Serikali kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya pamoja kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ ili kuwasaidia waathirika wa matukio hayo.
 Christina Onyango kutoka dawati la kijinsia kituo cha Polisi Stakishari (kulia) akimsikiliza mteja aliyekwenda kupata huduma kwenye kituo cha usuluhishi (CRC) ikiwa ni katika mikakati ya kupinga na kudhibiti ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na kutoa huduma ya elimu kwa wananchi.
 Wananchi wakisubiri huduma kutoka kituo  cha usuluhishi (CRC).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad