HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 8 December 2017

PROFESA MBARAWA: UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA UMEGHARIMU SHILINGI BILIONI 560Waziri wa ujenzi  uchukuzi na mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa amefanya  ukaguzi   wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la 3 la abiria la kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere   (JNIA)  ambao unatarajia kukamilika ifikapo mwakani .
 Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya ndege Juliuas  Nyerere  (JNIA) profesa Mbarawa amesema kuwa  ujenzi huo ambao umefikia asilimia 67 kukamilika umegharimu  takribani shilingi bilioni 560 katika ujenzi wake hadi sasa.
Aidha waziri huyo ametanabaisha kuwa  jengo hilo la 3 la abiria litakuwa na uwezo wa kuhifadhi ndege kubwa 11 ambapo huchukua abiria mia 300 hadi 400 na  ikiwa kwa ndege ndogo daraja c ni 21  nazo huchukua abiria 120-160 kwa kila moja.
Hata hivyo profesa Mbarawa amesema kuwa abiria wataondokana na changamoto ya kuchukua muda mrefu  katika kitengo cha uhamiaji pale wanapolazimika kufanyiwa ukaguzi  kutakuwa na mabadiliko ya kisasa  ya wahudumu  24  watakaokuwa wanahudumia abiria hao kwa muda usiopungua dakia 20 ili kuondokana na usumbufu pamoja na kuboresha huduma hizo .
Vile vile Mkurugenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa Richard Mayongela  ( DRA)  amesema kuwa abiria watapata huduma za viwango vya kimataifa ikiwa pia na  kufungwa  mitambo ya kisasa ili kudhibiti uhalifua utakojitokeza ikiwemo kusafirisha nyaraka za serikali bila kibali maalumu.
Mkurugenzi mayongela amemalizia kwa kusema  kuwa kutakuwa na fursa za wafanya biashara  mara baada ya jengo hilo kumalizika na kuwataka  wawekezaji kuchangamkia  fursa hiyo ikiwa ni mojawapo ya kuiingizia kipato mradi huo .
 aziri wa ujenzi  uchukuzi na mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la 3 la abiria leo Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere   (JNIA).
 Mkurugenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa Richard Mayongela  ( DRA) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa hapa nchini kuhusu uwanja huo utakavyokuwa wa kisasa na huduma bora leo Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere   (JNIA).
Wadau mbalimbali hapa nchini waliohudhuria mkutano huo wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la 3 la abiria leo Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere   (JNIA).
 Waziri wa ujenzi  uchukuzi na mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la 3 la abiria leo Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere   (JNIA).
 Waziri wa ujenzi  uchukuzi na mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa akiteta jambo na Mkurugenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa Richard Mayongela  ( DRA)  leo Jijini Dar es Salaam katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere   (JNIA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad